-
Mgogoro mkubwa waendelea 'Israel;' maandamano ya "Kupambana na Udikteta" yafanyika maeneo 130
Mar 09, 2023 22:55Kuanzia asubuhi ya jana Alkhamisi, maelfu ya Wazayuni wamemiminika mitaani kushiriki maandamano makubwa zaidi dhidi ya Netanyahu yaliyopewa jina la "Kupambana na Udikteta." Waandamanaji wamefunga barabara kuu zinazoelekea Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion, kujaribu kumzuia Waziri Mkuu wa utawala huo asiende Italia.
-
Arab League yaitaka jamii ya kimataifa kusitisha mauaji ya Israel huko Jenin
Mar 09, 2023 07:29Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imeitaka jamii ya kimataifa kusitisha mauaji na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina hususan katika eneo la Jenin.
-
Ansarullah: Mazungumzo yakivunjika tutaingia kwenye vita vya kuamua hatima ya Yemen
Mar 09, 2023 03:11Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema iwapo mazungumzo ya hivi sasa na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia yatafeli, vita vikali vitaanza vya kuhitimisha uchokozi na uvamizi huo.
-
Walowezi wa Kizayuni kwa mara nyingine wavamia msikiti wa al-Aqswa
Mar 08, 2023 23:06Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikkali wameuvamia tena Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuuvunjia heshima msikiti huo mtakatifu.
-
Kuongezeka hitilafu ndani ya jeshi na kuimarika uwezekano wa mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Netanyahu
Mar 08, 2023 23:02Katika kukabiliana na maandamano ya hivi karibuni, uasi na ukaidi wa askari wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala huo haramu, ameonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinatishia "misingi muhimu ya Israel" na kwamba tabia hiyo itaenea haraka katika mfumo mzima wa utawala huo.
-
'Pango la Simba' kulipiza kisasi cha mauaji ya Wapalestina Jenin
Mar 08, 2023 06:23Kundi la Muqawama wa Kiislamu la Arin al Usud (Pango la Simba) limesema litalipiza kisasi cha mauaji ya kikatili ya Wapalestina katika mji wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Hamas: Jinai za utawala wa Kizayuni hazitawatia hofu watu wa Wapalestina
Mar 08, 2023 03:06Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa taarifa ikiilaani jinai za Wazayuni huko Jenin na kusisitiza kuwa: Jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na mauaji yake dhidi ya raia wa Palestina kamwe hazitalitia hofu taifa hilo.
-
Iran kushiriki kikao cha pande nne cha kuratibu kuanzishwa tena uhusiano wa Uturuki na Syria
Mar 07, 2023 22:54Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ametangaza kuwa, maandalizi ya mkutano wa pande nne utakayohudhuriwa pia na Iran kwa ajili ya kuanzishwa tena uhusiano kati ya Uturuki na Syria yanaendelea.
-
Rais wa Palestina: Walimwengu chukueni hatua za kuzuia ugaidi wa Israel
Mar 07, 2023 22:53Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameitaka jamii ya kimataifa kukomesha ugaidi wa Israel na kufanya juhudi za kuhitimisha uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu unaofanywa na utawala huo wa Kizayuni.
-
Nasrullah: Matukio ya sasa yanaashiria hakika ya kusambaratika Israel
Mar 07, 2023 04:05Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema matukio na maendeleo yanayoshuhudiwa hivi sasa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni ishara tosha kuwa suala la kuporomoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni hakika ambayo itafanyika katika mustakabali wa karibu.