-
Maiti zingine 51 za Wapalestina waliouliwa shahidi na jeshi la kizayuni zagunduliwa Ghaza
Nov 14, 2025 04:13Timu za uokoaji za Palestina katika Ukanda wa Ghaza zimegundua na kufukua maiti zingine 51 za Wapalestina waliouliwa shahidi na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Vitisho vya mzayuni vyaifanya serikali ya Al-Jolani ifute maadhimisho ya Kimbunga cha Al-Aqsa
Nov 14, 2025 04:08Duru za habari zimeripoti kuwa kongamano la Operesheni ya Muqawama wa Palestina dhidi ya utawala wa kizayuni wa Israel ya Kimbunga cha Al-Aqsa, lililokuwa limepangwa kufanyika katika mji wa Aleppo nchini Syria limefutwa baada ya mwandishi mmoja wa habari wa Kizayuni kutoa vitisho kwa kiongozi wa mpito wa nchi hiyo, Al-Jolani na serikali yake.
-
Maafa ya vita vya kinyama vya Israel yamepelekea Wapalestina 6,000 wa Ghaza kukatwa viungo
Nov 13, 2025 23:07Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetoa ripoti inayoonyesha kuwa, Wapalestina 6,000 wamekatwa viungo katika eneo hilo tangu utawala wa kizayuni wa Israael ulipoanzisha vita vya kinyama Oktoba 2023 ambavyo vimeendelea kwa muda wa miaka miwili.
-
UN: Raia 114 wameuawa Lebanon katika ukiukaji wa usitishaji vita uliofanywa na Israel
Nov 13, 2025 23:07Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema ukiukaji wa usitishaji vita uliofanywa Israel uliotokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya utawala huo wa kizayuni na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon ya Hizbullah mnamo Novemba 2024 umesababisha vifo vya raia 114 wa nchi hiyo.
-
Mgogoro wa kisaikolojia miongoni mwa wanajeshi wa Israel; Wizara ya Vita ya Israel: Kujiua wanajeshi ni kielelezo cha kushindwa
Nov 13, 2025 22:54Gazeti la Uingereza The Independent, limeashiria ongezeko la kiwango cha kila mwaka cha kujiua katika jeshi la Israel baada ya vita vya Gaza, na kuandika kuwa: "Zaidi ya wanajeshi 11,000 wa Israel wamekumbwa na aina mbalimbali za matatizo ya kisaikolojia baada ya vita hivyo, na takwimu kuhusu wanajeshi wanaojiua baada ya kuondoka jeshini hazijachapishwa."
-
Al-Sudani asema, ataanza kufanya mazungumzo ya kuunda serikali mpya ya Iraq
Nov 13, 2025 08:55Waziri Mkuu wa Iraq Mohammad Shia al-Sudani amesema, ataanza kufanya mazungumzo hivi karibuni kwa ajili ya kuunda serikali mpya wakati muungano wake unaonekana kuongoza katika uchaguzi wa bunge.
-
Ujerumani ni muuzaji mkubwa wa pili wa silaha kwa Israel
Nov 12, 2025 23:07Imeelezwa kuwa, Ujerumani inashika nafasi ya pili duniani kwa kuuuzia silaha utawala haramu wa Israel unaofanya mauaji ya kinyama dhidi ya Wapalestina.
-
HAMAS: Silaha za Muqawama haziwezi kujadiliwa kabla ya kuundwa kwanza nchi ya Palestina
Nov 12, 2025 08:40Osama Hamdan, kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, amesisitiza kwamba, silaha za Muqawama ni suala lisiloweza kujadiliwa kabla ya kuundwa nchi dola ya Palestina na akabainisha kuwa, lengo la kisiasa la Muqawama litabaki kuwa ni kuikomboa ardhi, kuundwa nchi huru ya Palestina ambayo mji mkuu wake ni Baitul-Muqaddas na kuwepo hakikisho la kurejea wakimbizi.
-
Katibu Mkuu wa UN apongeza uchaguzi wa bunge Iraq, ahimiza kuundwa serikali kwa njia ya amani
Nov 12, 2025 07:42Wakati zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa Bunge la Iraq lingali linaendelea, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wananchi wa nchi hiyo kwa ushiriki wao katika uchaguzi huo na kuipongeza pia Tume Huru ya Uchaguzi (IHEC) kwa kuendelesha zoezi hilo kwa ufanisi.
-
Ni yepi matokeo ya kujiuzulu waziri wa mikakati wa utawala wa Kizayuni?
Nov 12, 2025 05:16Waziri wa masuala ya mikakati wa utawala wa Kizayuni na ambaye ni mtu wa karibu na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, amejiuzulu. Ron Dermer, ametangaza kujiuzulu kwa kumtumia barua rasmi Netanyahu.