-
Hamas: Kumbukumbu ya kuuawa Arafat ni kielelezo cha mwendelezo wa uhalifu wa Israel
Nov 12, 2025 02:32Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kwamba maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya kuuawa Rais wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat, yanatukumbusha kwamba "uhalifu wa kuzingirwa uliomlenga Arafat bado unaendelea dhidi ya watu wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza."
-
Hizbullah yasema silaha ni muhimu kwa ulinzi wa Lebanon, haitasalimu amri kwa Marekani au Israel
Nov 12, 2025 01:54Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kwamba wito wa Marekani na Israel wa kupokonya silaha kundi hilo la mapambano na muqawama unakusudiwa kuidhoofisha Lebanon na kuiacha ikikabiliwa na uvamizi wa kigeni.
-
Hamas yalaani mswada wa kifashisti na kikatili wa Bunge la Israel wa kuwanyonga Wapalestina
Nov 11, 2025 23:02Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Wapalestina, Hamas, imelaani vikali hatua ya Bunge la Israel (Knesset) kupitisha kwa mara ya kwanza mswada unaoruhusu kunyongwa kwa Wapalestina waliotekwa, ikikitaja kama mwendelezo wa sera za kibaguzi na jinai za utawala wa Kizayuni.
-
WHO: Zaidi ya wagonjwa 16,000 huko Gaza wanasubiri kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu
Nov 11, 2025 07:15Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa wagonjwa wasiopungua 16,500 katika Ukanda wa Gaza wanasubiri kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu na kusisitiza kuwa suhula zake za tiba ziko tayari mpakani lakini haziwezi kuingia katika eneo hilo kufuatia Israel kufunga vivuko hivyo.
-
UN: Israel inaendelea kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza
Nov 11, 2025 04:07Umoja wa Mataifa umesema Israel inaendelea kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia huko Gaza; mwezi mmoja baada ya kuanza kutekelezwa makualiano ya kusimamisha vita.
-
Waandishi habari 44 kati 270 waliouawa na Israel huko Gaza waliuawa wakiwa kwenye mahema ya wakimbizi
Nov 10, 2025 06:21Kundi la kutetea haki za waandishi wa habari wa Palestina limeripoti kuwa jeshi la Israel limewaua waandishi wa habari 44 wa Palestina katika mahema ya wakimbizi huko Gaza, wakiwa kati ya zaidi ya wafanyakazi 270 wa vyombo vya habari waliouawa na utawala huo katika eneo linalozingirwa la Ukkanda wa tangu Oktoba 2023.
-
HAMAS: Lengo la safari ya rais wa Israel Afrika ni kubadilisha misimamo ya nchi zinazounga mkono Palestina
Nov 10, 2025 02:48Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa safari ya rais wa utawala ghasibu wa kizayuni katika nchi za Afrika ni jaribio la kutaka kubadilisha msimamo wa nchi hizo wa zinazopinga ukoloni na kuunga mkono haki za watu wa Palestina.
-
Afisa wa Yemen: Mtandao wa ujasusi wa Marekani, Israel na Saudi Arabia unataka kukomesha himaya ya Yemen kwa Palestina
Nov 09, 2025 08:19Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amevipongeza vikosi vya usalama vya nchi hiyo kwa kuvunja mtandao wa ujasusi uliounganishwa na mashirika ya ujasusi ya Marekani, Israel na Saudi Arabia, akisema kuwa kundi hilo la ujasusi lilitaka zaidi kupunguza uungaji mkono na himaya ya serikali ya Sana'a kwa Palestina.
-
Israel yaua watu watatu Kusini mwa Lebanon baada ya kutishia mashambulizi mapya ya kijeshi
Nov 09, 2025 04:01Jeshi la Israel limewaua watu watatu katika maeneo ya kusini mwa Lebanon kupitia mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa kwa nyakati tofauti, siku chache tu baada ya kutoa onyo la kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya taifa hilo jirani.
-
Iraq yaanza upigaji kura maalum wa uchaguzi wa bunge kwa wanajeshi na wakimbizi
Nov 09, 2025 03:50Mchakato wa upigaji kura maalum kwa ajili ya wanajeshi na wakimbizi katika uchaguzi wa bunge la Iraq umeanza rasmi leo Jumapili katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.