-
Hamas yatuma salamu za hongera kwa kuachiwa huru mwanamapambano wa Kijapani
May 29, 2022 07:46Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina zimetuma salamu za hongera kwa kuachiwa huru Fusako Shigenobu, mwanamama mtetezi na muungaji mkono wa Palestina ambaye alitumikia kifungo cha miaka 20 katika jela za Japan.
-
Oman yasisitiza msimamo wa kutoanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel
May 29, 2022 03:06Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman siku ya Jumamosi alitangaza kuwa nchi yake haitaanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel huku akitoa wito wa kutatuliwa kwa haki suala la Palestina.
-
Khatibu wa Msikiti nwa al-Aqswa: "Maandamano ya Bendera" katu hayataingia Masjidul-Aqswa
May 28, 2022 22:55Khatibu wa Masjidul-Aqswa amesema kuwa, uamuzi wa Wazayuni wa kufanya "Maandamano ya Bendera" ni hatua ya kichochezi na amesisitiza juu ya udharura wa kuchukuliwa hatua ya kuwazuia Wazayuni hao kuingia katika msikiti matakatifu wa al-Aqswa.
-
HAMAS: "Maandamano ya Bendera" yasipoghairishwa yamkini tukatoa jibu kwa kombora
May 28, 2022 03:25Kiongozi mmoja mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, "ikiwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hautaacha uvamizi wake dhidi ya msikiti wa Al Aqsa na hautaghairisha maandamano ya bendera, katika hali hiyo tutafikisha ujumbe wetu kwa kombora."
-
Hatua muhimu mno ya kiistratijia ya Bunge la Iraq; uhusiano wowote na Israel ni uhalifu
May 28, 2022 02:40Juzi Alkhamisi tarehe 26 Mei, 2022, Bunge la Iraq lilipasisha kwa kauli moja sheria ya kutambua kuwa ni uhalifu, hatua yoyote ya kuweka uhusiano wa kawaida baina ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Bunge la Iraq lapasisha sheria ya kupiga marufuku kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel
May 27, 2022 06:40Bunge la Iraq limepasisha kwa kauli moja sheria ya kupiga marufuku ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
-
Russia yakosoa uvunjaji sheria wa Israel na hatua yake ya kupora ardhi za Wapalestina
May 27, 2022 06:39Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa amekosoa hatua ya Israel ya kuendelea kukiuka sheria, kupora ardhi za Palestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.
-
Utawala wa Kizayuni wa Israel, utawala wa mauaji
May 27, 2022 04:40Gazeti la Marekani la New York Times limeripoti kuwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel umeitaarifu Marekani kwamba ndio uliohusika na mauaji ya Shahidi Hassan Sayyad Khodaei.
-
Muqawama wa Palestina: Maandamano ya bendera ya Wazayuni yatawasha moto
May 27, 2022 02:28Makundi mbalimbali ya mapambano ya Kiislamu ya Palesitna yametoa mwito kwa Wapalestina kujitokeza kwa wingi kuulinda Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu, kama ambavyo pia yameonya kuhusu hatari ya maandamano ya bendera ya utawala wa Kizayuni kwa usalama wa eneo hili.
-
Jihadul-Islamu ya Palestina yalaani vikali safari ya waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Israel
May 26, 2022 22:03Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina imelaani vikali safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kukutana na viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.