-
Kwa nini ni lazima Marekani iondoke Asia Magharibi?
Aug 11, 2026 07:54Uwepo wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi, ambao kwa miaka mingi umehalalishwa kwa kisingizio cha kudhamini usalama, sasa umekuwa kichocheo cha migogoro, sababu ya kuongezeka gharama, na jambo linaloitumbukiza Washington katika vita vya kuchosha na vya muda mrefu, kuliko wakati mwingine wowote.
-
Mustakabali wa usalama wa eneo: Kwa nini nafasi muhimu ya nchi za kanda ni ya dharura?
Aug 11, 2026 07:25Pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa ajili ya kutetea Quds Tukufu (Jerusalem), uliofanyika mjini Amman, Jordan, Badr Abdelatty, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, alisisitiza umuhimu wa kuandaliwa dira ya pamoja ya Kiarabu kwa ajili ya mustakabali wa usalama wa eneo. Alisema kuwa nchi za eneo lazima ziwe katika mstari wa mbele wa kubuni mipango yoyote ya usalama katika siku zijazo.
-
Kiwango cha mimba zinazoharibika Gaza chaongezeka mara tatu katika nusu ya kwanza ya 2026
Aug 11, 2026 03:02Kiwango cha mimba kuharibika huko Gaza kimeongezeka zaidi ya mara tatu katika nusu ya kwanza ya 2026 huku wanawake wajawazito wakisumbuliwa na utapiamlo, kuhama makazi yao mara kwa mara, joto kali na kuendelea kuporomoka mfumo wa afya wa Ukanda huo.
-
Karibu Wapalestina 8,000 wamekatwa viungo katika vita vya Israel dhidi ya Gaza
Aug 10, 2026 11:17Wapalestina wapatao 8,000 wamekatwa viungo katika eneo la Ukanda wa Gaza tangu utawala wa kizayuni wa Israel ulipoanzisha vita vya kinyama Oktoba 2023 ambavyo vimeendelea kwa Zaidi ya miaka miwili.
-
Francesca Albanese: Mauaji ya kimbari na Apartheid vimekuwa sera rasmi ya utawala wa Israel
Aug 10, 2026 10:51Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu Francesca Albanese amesema kuwa, mauaji ya kimbari na mfumo wa ubaguzi wa rangi (apartheid) vimegeuzwa kuwa mradi wa kiserikali wa utawala wa Israel.
-
Jeshi la Yemen laangamiza makumi ya mamluki wa Saudia mkoani Ta'izz
Aug 10, 2026 03:15Msemaji wa Vikosi vya Jeshi la Yemen amesema vitengo vya kijeshi vya nchi hiyo vimeendesha operesheni kubwa dhidi ya vibaraka wa Saudia katika mkoa wa kusini-magharibi wa Ta’izz, na kuwaua na kuwajeruhi makumi yao.
-
Yemen yavishambulia vituo vya nishati vya Saudi baada ya nchi hiyo kukiuka anga ya Sa’adah na Hajjah
Aug 09, 2026 11:00Yemen imeishambulia miundombinu ya nishati ya Saudi Arabia ikiwa ni jibu kwa ndege zisizo na rubani za adui zinazokiuka anga ya mikoa ya Sa’adah na Hajjah huko Yemen.
-
Malaysia na Indonesia zasisitiza kuunga mkono Palestina na maeneo matakatifu Baytul-Muqaddas
Aug 09, 2026 03:15Malaysia na Indonesia kwa mara nyingine tena zimesisitiza uungaji mkono wao kwa watu wa Palestina na kuhifadhi hadhi ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo katika Baytul-Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
-
UNICEF yachukua hatua dhidi ya afisa anayetuhumiwa kufanya ujasusi kwa maslahi ya Israel
Aug 09, 2026 02:58Msemaji wa Umoja wa Mataifa amethibitisha kwamba Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) linachukua hatua dhidi ya mmoja wa wafanyakazi wake, kufuatia madai kwamba alifanya ujasusi kwa maslahi ya Israel wakati wa kazi yake ya awali katika Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa.
-
Ansarullah: Baraza la Usalama la UN limepoteza hadhi; maazimio yake hayana thamani
Aug 08, 2026 12:50Kiongozi mwandamizi wa harakati ya Ansarullah nchini Yemen amepuzilia mbali hatua ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kulaani mashambulizi ya makombora ya kulipiza kisasi dhidi ya Saudi Arabia na meli za kibiashara za utawala huo wa kifalme akisema kuwa chombo hicho cha kimataifa kimepoteza uhalali na hadhi yake, na maazimio yake hayana thamani yoyote.