Jul 28, 2023 02:25 UTC
  • Nafasi ya utawala wa Kizayuni katika kueneza chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi

Tangu kuasisiwa kwake, utawala ghasibu wa Kizayuni sambamba na kupora ardhi za Wapalestina, umefanya jinai zisizohesabika dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina, pamoja na kuchochea vita na ukosefu wa amani na usalama katika eneo la Asia Magharibi.

Utawala huo ghasibu umekuwa ukifanya njama za kupambana na Uislamu na kueneza vita vya kisaikolojia na kipropaganda dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ili kufikia lengo hilo umekuwa ukitumia pesa nyingi kwa madhumuni ya kudhamini mahitaji na malengo ya wale wanaopigana na kuuharibia jina Uislamu.

 

Salwan Momika

Njama hizo za uhasama wa Israel sasa zinaonekana wazi katika vitendo vya kuupiga vita Uislamu na matukufu ya Waislamu huko Ulaya, haswa uchomaji wa Qur'ani katika nchi za Ulaya Kaskazini, ambazo ni Sweden na Denmark. Siku ya Alhamisi, Julai 20, kwa mara ya pili katika wiki chache zilizopita, Salwan Momika, mhalifu aliye na uraia wa Iraq na Uswidi, aliivunjia heshima Qur'ani Tukufu kwa msaada wa polisi wa nchi hiyo ya Ulaya, kitendo cha uchochezi ambacho kilizikasirisha sana nchi za Kiislamu. Kabla ya hapo, Jumatano Juni 28, wakati wa maadhimisho ya Eid al-Adha, Salwan Momika alichoma moto Qur'ani Tukufu, mbele ya macho ya Waislamu wapatao 200, nje ya msikiti mkuu huko Stockholm, huku akiungwa mkono na kulindwa na maafisa na polisi wa Uswidi. Kudhalilishwa huko kwa Qur'ani Tukufu kulikabiliwa na malalamiko makali ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kuhusiana na hilo, Wizara ya Intelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilichapisha taarifa mpya inayothibitisha kufungamana kibaraka huyo aliyevunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden na utawala wa kibaguzi wa Israel. Baada ya tangazo hilo la Julai 10 Wizara ya Intelijensia ya ilikamilisha tangazo hilo kwa taarifa na yingine iliyochapishwa Julai 25 ambapo ilisema kuwa kwenda sambamba mradi wa jinai ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na Salwan Momika nchini Sweden na mashambulizi ya kichokozi ya Wazayuni huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na hasa Jenin, pamoja na hali ya mgogoro ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, kunaonyesha udhalilishaji huo wa Qur'ani ulipangwa kwa makusudi na Wazayuni ili kupotosha fikra za waliowengi katika ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na mashambulizi hayo ya kinyama dhidi ya Wapelestina wasio na hatia.

Maandamano ya kutetea Qur'ani Tukufu nchini Iran

Mnamo 2019, shirika la ujasusi la Israeli Mossad, lilimuajiri rasmi Momika na kumpa jukumu la kukusanya habari za siri na za kijasusi kutoka kwa Waslamu wa Iraq. Baada ya kuihudumia Mossad kwa muda mrefu, Momika aliomba ahamishiwe katika nchi ya Ulaya. Makachero wa utawala wa Kizayuni walikubali ombi hilo kwa sharti kwamba aendelee kutekeleza operesheni yoyote atakayopewa na makechero hao, na ndipo wakamwombea makazi na uraia wa Uswidi. Kwa msingi huo, ni wazi kuwa Momika kupewa makazi huko Uswidi ni njama iliyopangwa siku nyingi nyuma kwa madhumuni ya kutekeleza mradi wa kueneza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Hii si mara ya kwanza kufichuliwa njama ya utawala wa Kizayuni kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na watu wenye chuki na uhasama dhidi ya Uislamu. Mbali na utawala huo wa kigaidi kutekeleza hatua za chuki dhidi ya Uislamu, kama vile kufanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa, Qibla cha kwanza cha Waislamu na waumini wa Kipalestina, ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa idadi kubwa miongoni mwao, utawala huo umekuwa ukifanya juhudi kubwa za kubadilisha muundo na utambulisho halisi wa Kiislamu wa eneo hilo takatifu. Hatua kama vile za kuchimba mahandaki na njia za chini kwa chini chini ya Msikiti wa al-Aqsa kwa kisingizio cha kufuatilia masuala ya kiakiolojia, kwa hakika zinachukuliwa kwa lengo la kuliharibu jengo hilo takatifu. Vilevile tarehe 21 Juni baadhi ya walowezi wa Kizayuni waliokuwa wamevalia maski usoni walivunjia heshima Qur'ani Tukufu huko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuteketeza moto shule, nyumba kadhaa na msikiti katika eneo hilo.

Nasser Kanani

Katika kujibu udhalilishaji huo wa Wazayuni dhidi ya Qur'ani Tukufu, Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema: "Shambulio la kikatili la Wazayuni kwenye misikiti na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu, kuharibiwa nyumba, mauaji ya kila siku ya watoto na wanawake na watu wasio na ulinzi wa Palestina ni ishara kwamba utawala huo bandia hauna mipaka yoyote katika uchokozi na kuvunjia heshima matukufu ya kidini na haki za binadamu.”

Katika uga wa kueneza chuki dhidi ya Uislamu, mabepari na studio za filamu zenye mafungamano na utawala wa Kizayuni hususan huko Hollywood zinafanya juhudi kubwa za mfululizo za kutengeneza filamu bandia ambazo zinaonyesha sura ya kutisha na isiyo ya kibinadamu ya Uislamu na Waislamu. Vile vile, katika kueneza njama za maadui wa Uislamu, utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake na hasa Marekani wanawekeza na kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kueneza chuki na kuchafua jina zuri la Uislamu kwa kuutuhumu kuwa unaunga mkono ugaidi. Nchi za Magharibi zinaeneza propaganda nyingi bandia na kuuhusisha Uislamu na ugaidi na kuutuhumu kuwa ni tishio kwa walimwengu, ili kuandaa mazingira ya kukandamizwa Waislamu na kuenezwa chuki dhidi ya dini yao tukufu. Vitendo hivyo vinatekelezwa kupitia mbinu kama vile za kuchomwa moto Qur'ani na kudhalilishwa Mtume Mtukufu (saw) kwa kuchapishwa vikatuni vya matusi katika jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo.

 

Tags