Afrika Kusini yaitaka jamii ya kimataifa iwasaidie wananchi wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i111650-afrika_kusini_yaitaka_jamii_ya_kimataifa_iwasaidie_wananchi_wa_gaza
Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutoa uamuzi wa dharura wa kuwaunga mkono Wapalestina huko Rafah.
(last modified 2024-05-11T09:14:37+00:00 )
May 11, 2024 09:14 UTC
  • Afrika Kusini yaitaka jamii ya kimataifa iwasaidie wananchi wa Gaza

Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutoa uamuzi wa dharura wa kuwaunga mkono Wapalestina huko Rafah.

Katika sehemu nyingine ya taarifa yake, Afrika Kusini imeitaka jamii ya kimataifa kutopuuza mauaji ya kimbari huko Gaza yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel.

Hayo yamo katika taarifa ya Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini ambayo imesisitiza kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Haki inapaswa kutoa amri ya dharura ya kuwaunga mkono Wapalestina baada ya shambulio la Israel dhidi ya mji wa Rafah.

Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuitaka Israel isitishe mashambulizi yake dhidi ya Rafah na kuwezesha kuingia kwa maafisa wa Umoja wa Mataifa katika mji huo.

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ)

 

Itakumbukwa kuwa serikali ya Afrika Kusini imefungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mauaji yake ya kimbari huko Gaza.

Afrika Kusini ambayo ilipitia kipindi kigumu cha mateso na manyanyaso ya utawala wa makaburu weupe, imekuwa mstari wa mbele kuwatetea Wapalestina wanaouawa kikatili wa Ukanda wa Gaza.

Jeshi katili la Israel limeua takriban Wapalestina 35,000 huko Gaza tangu tangu lianzishe mauaji ya kimbari dhidi ya eneo hilo  Oktoba 7 mwaka jana. Idadi kubwa ya waliouawa ni wanawake na watoto.