Aug 09, 2023 03:12 UTC
  • Tofauti zapamba moto baina ya Republican na Democrats kuhusu kesi ya mtoto wa Biden

Chama cha Republican kimekosoa waziwazi mienendo ya kindumakuwili ya mfumo wa mahakama na Rais wa Merekani kuhusu kesi inayomkabili mtoto wa Joe Biden.

Ni baada ya kupita miaka isiyopungua kumi sasa tangu kuibuliwa faili la kesi ya mtoto wa kiume wa Rais Joe Biden wa Marekani, Hunter Biden, kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, kupokea rushwa na kukwepa kulipa kodi. 

Kevin McCarthy, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, amekosoa waziwazi mienendo ya kindumakuwili ya mfumo wa mahakama na rais wa nchi hiyo na kusema kuwa, serikali ya Marekani hairuhusu Hunter Biden ahukumiwe kwa makosa yake mengi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani hivi majuzi aliashiria ripoti ya Idara ya Huduma za Ndani ambayo inaonyesha kuwa, wanashughulikia kwa mwendo wa kinyonga uchunguzi wa uhalifu wa kukwepa kodi wa Hunter Biden.

Uchunguzi wa Baraza la Wawakilishi la Marekani umegundua kuwa mamilioni ya fedha kutoka nje ya nchi ziliwekwa kwenye akaunti za wanafamilia wa Joe Biden na washirika wake kupitia makampuni feki.

Joe na Hunter Biden

Ikulu ya Rais wa Marekani imejibu matamshi hayo ya Spika McCarthy ikiwashutumu Warepublican katika Baraza la Wawakilishi kuwa hawazingatii masuala muhimu ya nchi.

Mwezi Juni mwaka huu pia barua pepe zilizofichuliwa na kampuni ya gesi ya Ukraine zilionyesha kuwa, Rais wa Marekani, Joe Biden na mwanawe Hunter Biden walishiriki katika utakatishaji fedha wa kampuni hiyo. Kulingana na yaliyomo katika ripoti hizo zilizovuja, mmiliki wa kampuni ya Ukraine alituma dola milioni 10 kwa Hunter na baba yake, Joe Biden.

Tags