112 wapoteza maisha katika mafuriko nchini China
https://parstoday.ir/sw/news/world-i10642-112_wapoteza_maisha_katika_mafuriko_nchini_china
Kwa akali watu 112 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko na vimbunga vilivyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katikati na kusini mwa China.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 05, 2016 13:28 UTC
  • 112 wapoteza maisha katika mafuriko nchini China

Kwa akali watu 112 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko na vimbunga vilivyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katikati na kusini mwa China.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema watu milioni 16 wameathiriwa na majanga hayo ya kimaumbile na haswa baada ya Mto Yangtze, ambao ni mrefu zaidi nchini China kuvunja kingo zake.

Aidha idadi kubwa ya watu wanaoishi katika fukwe za Ziwa Taihu karibu na mji wa Shanghai wamepoteza maisha kutokana na mafuriko hayo. Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa, yumkini walioaga dunia kutokana na athari za mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini China imepindukia watu 180.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya China imeripoti kuwa, hekari milioni 1.34 za mazao zimeharibiwa na mafuriko hayo na kuathiri pakubwa sekta ya kilimo.

Itakumbukwa kuwa, zaidi ya watu 4,000 walifariki dunia kutokana na mafuriko katika eneo la Yangtze nchini China mwaka 1998.