May 08, 2024 11:39 UTC
  • Wataalamu wa hali ya Hewa: Mwezi Aprili dunia iliathiriwa na joto kali

Kitengo cha ufuatiliaji wa hali ya hewa cha Ulaya kimeeeleza kuwa dunia ilikumbwa na joto kali mwezi Aprili mwaka huu; kiwango ambacho kimetajwa kuwa ni muendelezo mtawalia wa hali ya joto kali kwa muda wa miezi 11 ambayo haijawahi kushuhudiwa.

Kiwango hicho kikubwa cha joto kimeshuhudiwa licha ya kudhoofika kwa El Nino; wimbi la hali ya hewa ambalo hupasha joto Bahari ya Pasifiki na kusababisha ongezeko la joto duniani. 

Wimbi la hali ya hewa ya El Nino 

Mwezi Aprili mwaka huu ulikuwa na ongezeko la joto la nyuzi 1.58. Ingawa kuna mabadiliko ya hali ya joto yanayohusiana na mizunguko ya asili kama vile El Nino; lakini imeelezwa kuwa nishati ya ziada iliyonaswa ndani ya bahari na angahewa ambayo huongeza viwango vya gesi chafu itaendelea kusukuma joto la dunia kuelekea rekodi mpya. Haya yameelezwa na Carlo Buontempo wa Taasisi ya The Copernicus Climate Change Service.  

Hii ni katika hali ambayo wastani wa halijoto katika kipindi cha miezi 12 iliyopita ulivuka kiwango muhimu cha ongezeko la joto cha 1.5C (2.7F) kilkichoainishwa katika Mtakaba wa Mabadiliko ya Tabianchi ya Paris  2015.

Mwaka 2015 karibu serikali 200 duniani zilisaini makubaliano hayo ili kuondoa matumizi ya nishati ya fosili itakayochukua mbadala wa nishati katika nusu ya pili ya karne.