Korea Kusini kupanua ushirikiano wake na bara la Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i112558-korea_kusini_kupanua_ushirikiano_wake_na_bara_la_afrika
Korea Kusini jana ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Kiafrika ambao wamewakilishwa na wajumbe kutoka nchi 48 wakiwemo wakuu wa nchi wapatao 30.
(last modified 2024-06-04T23:44:33+00:00 )
Jun 04, 2024 23:44 UTC
  • Korea Kusini kupanua ushirikiano wake na bara la Afrika

Korea Kusini jana ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa viongozi wa Kiafrika ambao wamewakilishwa na wajumbe kutoka nchi 48 wakiwemo wakuu wa nchi wapatao 30.

Akihutubia mkutano huo wa Korea na bara la Afrika mjini Seoul, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema nchi misaada ya maendeleo barani Afrika hadi karibu dola bilioni 10 ifikapo mwaka 2030 na kwamba itapanuua ushirikiano wa kina hasa katika sekta muhimu za madini na teknolojia.

Leo, wakuu wa biashara wa Korea Kusini watafanya mkutano wa kilele wa biashara utakaojikita katika masuala ya uwekezaji, maendeleo ya viwanda na usalama wa chakula.

Rais wa Kenya, William Ruto alihutubia kongomano la kwanza la Korea na mataifa ya bara Afrika huku akisisistiza umuhimu wa nafasi ya Korea katika mageuzi ya Afrika.

Ruto amedokeza kuwa, Afrika ina nia ya kutathmini fursa ya uwekezaji na Korea ambayo ushirika huo utaunda nafasi za kazi na kusaidia kukuza uchumi.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongomano hilo, Rais Ruto amesema: “Mkutano huu unaonyesha azma ya kuinua uhusiano huu na kuhamasisha utashi wa kisiasa unaohitajika kwa Afrika na Korea Kusini kustawi pamoja kupitia ushirikiano wa kunufaisha pande zote mbili. Ili kufanya hivi, ni lazima tujitokeze kwenye nyongeza zetu na kutekeleza mikakati ya ushindi kwa msingi wa ushirikiano sawa,”

Viongozi kadhaa kutoka ukanda wa Afrika Mashariki nao wanahudhuria kongamano hili, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na Rais Paul Kagame wa Rwanda.