Wamarekani waandamana kulaani ugaidi wa Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11260-wamarekani_waandamana_kulaani_ugaidi_wa_saudia
Mamia ya Wamarekani wenye asili ya nchi za Mashariki ya Kati wamefanya maandamano mjini Washington kulaani uungaji mkono wa Saudi Arabia kwa makundi ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 14, 2016 23:41 UTC
  • Wamarekani waandamana kulaani ugaidi wa Saudia

Mamia ya Wamarekani wenye asili ya nchi za Mashariki ya Kati wamefanya maandamano mjini Washington kulaani uungaji mkono wa Saudi Arabia kwa makundi ya kigaidi.

Wanaharakati na waandamanaji hao wamekusanyika nje ya ubalozi wa Saudia mjini Washington na kisha kuandamana hadi katika Ikulu ya White House kulalamikia hatua ya Riyadh ya kuliunga mkono kundi la kigaidi la ISIS (Daesh).

Aidha wamefanya maandamano hayo kukosoa hatua ya utawala wa kifalme wa Aal Saud ya kuzivamia nchi za Kiislamu za Syria, Yemen, Bahrain na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Waandamanaji hao wamesikika wakipiga nara na shaari kama vile "Saudia, ISIS, ISIL, Daesh; wote ni kitu kimoja, tofauti ni majina tu."

Kadhalika waandamanaji hao wamesikika wakiitaka serikali ya Washington ikate uhusiano wake na Riyadh wakisisitiza kuwa, Saudia ndiyo mzizi na chimbuko la maovu yote Mashariki ya Kati.

Medea Benjamin, mmoja wa waandamanaji hao na mwanaharakati wa vuguvugu la Amani na Haki ya Kijamii amewaambia waandishi wa habari katika maandamano hayo kuwa: "Sote tunafahamu kuwa Saudia imekuwa ikieneza ugaidi, misimamo ya kufurutu ada na idiolojia za Kiwahabi Mashariki ya Kati na Kusini mwa Asia, lakini sasa inaeneza harakati hizo katika kona zote za duniani."