National Interest: Umewadia wakati sasa kwa Marekani kuacha kuipatia silaha Israel
Gazeti la National Interest limeandika katika moja ya makala yake kuhusiana na msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Israel na mzigo mkubwa wa gharama hizo unaotolewa na wananchi wa nchi hiyo na kutoa mwito wa kuhitimishwa msaada huo.
Katika makala iliyoangazia gharama za vita vya Gaza, ambavyo hulipwa na serikali ya Washington kwa kutumia fedha za kodi za Wamarekani kusaidia mashambulizi ya pande nyingi ya utawala wa Kizayuni, gazeti la National Interest limeandika: Wakati umefika wa kusimamisha upelekaji wa silaha wa Marekani hadi Tel Aviv.
Kwa mujibu wa jarida la Marekani la National Interest, uamuzi wa utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani wa kutuma mfumo wa ulinzi wa makombora wa THAAD na wanajeshi 100 wa Marekani kwa Israel kwa ajili ya operesheni na uungwaji mkono unaonyesha hatua za hivi karibuni zaidi za Washington katika kuunga mkono vita vya kila upande vya Tel Aviv katika eneo la Asia Magharibi.
Kwa mujibu wa chapisho hili la jarida hilo, gharama za usaidizi huu zinaongezeka kwa kasi na kutumwa kwa vikosi vya Marekani huko Israel huongeza hatari ya kuhusika moja kwa moja na Marekani katika vita.