Waislamu wana wasiwasi kuhusu ongezeko la ubaguzi katika nchi za Ulaya
(last modified Thu, 14 Nov 2024 02:43:30 GMT )
Nov 14, 2024 02:43 UTC
  • Waislamu wana wasiwasi kuhusu ongezeko la ubaguzi katika nchi za Ulaya

Shirika la Haki za Msingi la Umoja wa Ulaya limetangaza kwamba Waislamu wa bara hilo wameathiriwa na ongezeko kubwa la ubaguzi wa rangi na wana wasiwasi mkubwa.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya uchunguzi wa karibuni kwa Waislamu 10,000 katika nchi 13 za bara la Ulaya. 

Matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kuwa, nusu ya Waislamu wa bara Ulaya wanakabiliwa na mienendo ya chuki na ubaguzi unaoongezeka, ambao umeathiri nyanja mbalimbali za maisha yao, ikiwa ni pamoja na elimu, ajira na hata kukodisha nyumba.

Masoud Shajareh, Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kiislamu nchini Uingereza amesema: "Tumeandaa ripoti katika nchi za Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Canada, Marekani na Italia, ambazo zote zinaonyesha kuwa kumetengenezwa mazingira ambayo wanasiasa, waandishi wa habari, televisheni. watengenezaji programu na hata sinema za Hollywood na bidhaa zingine za kitamaduni katika nchi za Magharibi zinawasilisha Uislamu kwa sura hasi na mbaya.

Vilevile Wakala wa Haki za Msingi wa Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa, kushadidi ubaguzi dhidi ya Waislamu barani Ulaya kunafunganishwa na kushamiri vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia.

Vyama hivyo mara nyingi huiunga mkono Israel na kebeba bendera ya utawala wa Kizayuni katika mikutano yao.

Wakati huo huo, mashirika yanayofuatilia masuala ya kijamii nchini Uingereza yanaamini kuwa, baada ya watu hasa Waislamu kuunga mkono haki za Wapalestina na kupinga mauaji ya kimbari yanayofanywa dhidi yao, mashambulizi dhidi ya Waislamu barani Ulaya, ikiwemo Uingereza, yameongezeka, na Waislamu, mali na maeneo yao wanalengwa kwa mashambulizi ya kibaguzi.