CAIR yamjibu Papa: Mauaji ya kimbari ya Ghaza si ya kuchunguzwa, ni jambo lililo dhahiri
Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limekaribisha wito wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis wa kufanywa uchunguzi ili kubaini kama utawala wa Kizayuni umefanya mauaji ya kimbari ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, lakini limesisitiza kuwa hauhitajiki uchunguzi na uthibitisho kwa jambo lililo dhahiri.

Amefafanua: "nchi nyingi za Umoja wa Mataifa na mashirika yenye mamlaka ya kimataifa yamefikia hitimisho kwamba Israel inafanya mauaji ya kimbari. Kinachotakiwa ni kuchukuliwa hatua za kukomesha mauaji hayo".
Katika ujumbe alioweka kwenye X, Albanese amesema, anatumai kuwa Papa Francis atapata wakati wa kusoma ripoti mbili ambazo ameandika yeye mwaka huu, pamoja na ile ya Kamati ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Matendo ya Israel, "inayojumuisha mashtaka ya mauaji ya kimbari".
Ripota huyo wa UN ameongeza kuwa hata mwandishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula ametoa ripoti inayoshutumu uwekaji watu na njaa na kuharibu mamlaka na uhuru wa chakula kama kitendo cha mauaji ya kimbari.../