Kellogg: Marekani inataka 'kuvunja' muungano wa Russia na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i122800-kellogg_marekani_inataka_'kuvunja'_muungano_wa_russia_na_iran
Keith Kellogg Mjumbe maalumu wa Washington kwa ajili ya Ukraine na Russia amesema kuwa Marekani inataka kuvunja muungano uliopo kati ya Russia, Iran na China.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Feb 16, 2025 04:24 UTC
  • Kellogg: Marekani inataka 'kuvunja' muungano wa Russia na Iran

Keith Kellogg Mjumbe maalumu wa Washington kwa ajili ya Ukraine na Russia amesema kuwa Marekani inataka kuvunja muungano uliopo kati ya Russia, Iran na China.

Amesema, Marekani itafanya kila iwezalo kukata ushirikiano wa Russia na nchi mbili za Iran na China. Keith Kellogg alieleza haya jana akihutubia Mkutano wa Usalama wa Munich. 

Amedai kuwa muungano huu haukuwepo miaka minne iliyopita katika muhula wa kwanza wa urais wa Donald Trump. 

Mjumbe Maalumu wa Marekani kwa jaili ya Russia na Ukraine ameeleza hayo huku Iran na Russia zikiendelea kupanua ushirikiano wao wa kistratajia kupitia makubaliano ya muda mrefu na miradi mikubwa ya pande mbili iliyosainiwa na nchi mbili. 

Ushirikiano wa Russia na Iran umefikia katika kiwango cha juu katika miaka ya karibuni kufuatia nchi hizo kushirikiana katika nyanja za miundomsingi, nishati na masuala ya ulinzi. 

Mwezi uliopita, Tehran na Moscow zilisaini Makubaliano Makubwa ya Ushirikiano wa Kimkakati na hivyo kutayarisha uwanja wa ushirikiano wa muda mrefu katika miradi mbalimbali mikubwa katika kipindi cha miaka 20 ijayo. 

Weledi wa mambo wanasema kuwa  makubaliano hayo yamejikita katika dira ya pamoja kuelekea ulimwengu wa pande kadhaa na kupinga  sera za upande mmoja za Magharibi.