Tahadhari kuhusu kukamatwa wanafunzi wanaoiunga mkono Palestina nchini Marekani
Tovuti ya Axios imeonya kuhusu kuendelea kukamatwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanaoiunga mkono na kuitetea Palestina nchini Marekani.
Tovuti ya Axios imeandika kuwa: "Rumeysa Ozturk, mwanafunzi Mmarekani mwenye asili ya Uturuki katika Chuo Kikuu cha Tufts katika jimbo la Massachusetts, alikamatwa baada ya kuchapisha makala dhidi ya Israel kwenye gazeti la wanafunzi la chuo hicho akitaka kuheshimiwa "hadhi sawa na ubinadamu wa watu wote, ikiwa ni pamoja na Wapalestina."

Kukamatwa kwa Ozturk kunakuja huku kamatakamata ya utawala wa Donald Trump dhidi ya raia wengine halali wa Marekani ikiendelea kwa kasi kubwa, baada ya maafisa wa Marekani kutoa vitisho vya kuzitoza faini kampuni za sheria zinazowasaidia wahamiaji.
Wakati huo huo visa za masomo za zaidi ya wanafunzi 300 wa kigeni nchini Marekani zimefutwa katika muda wa wiki tatu zilizopita.
Kamatakamata hiyo hasa ya Wamarekani na wageni wanaopinga mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel huko Palestina na kukosekana taratibu za haki na uadilifu, vimewatia wasiwasi wataalamu kuhusu mwelekeo wa Marekani kwenye ufashisti na ubabe unaotumika nchini humo katika utawala wa Trump.