Luxembourg kuitambua Palestina katika Mkutano Mkuu wa UN
Serikali ya Luxembourg imetangaza mpango wake wa kulitambua taifa la Palestina, na hivyo kuungana na mataifa mbalimbali ya Ulaya ambayo yanatarajiwa kutoa tamko sawa na hili katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu.
Waziri Mkuu wa Luxembourg Luc Frieden na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Xavier Bettel wiki hii wameifahamisha kamisheni ya Bunge la nchi hiyo kwamba uamuzi wa mwisho utawekwa wazi kwa ushirikiano na Ufaransa, Ubelgiji na mataifa mengine.
Ripoti zinaeleza kuwa tangazo hili limepangwa kwenda sambamba na kikao cha Umoja wa Mataifa mjini New York ambapo viongozi wa nchi za Ulaya wanazamiwa kutangaza kulitambua rasmi taifa la Palestina.
Waziri Mkuu wa Luxembourg ametangaza mpango wa serikali ya nchi hiyo wa kulitambua taifa la Palestina baada ya serikali ya nchi hiyo kusitasita kwa miezi kadhaa na kujibu maombi yanayoongezeka kila uchao ya viongozi wa Uaya wanaotaka kusitishwa vita na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
Hadi saa Wapaelstina 64,905 wameuawa shahidi khususan wanawake na watoto.