Russia: Israel inapasa kuondoka katika ardhi ya Lebanon
-
Vasily Nebenzya. Mwakilishi wa Russia UN
Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kuwa Israel haiheshimu kivyovyote majukumu ya askari jeshi wa kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.
Vasily Nebenzya amesema kuwa Wazayuni wanawashambulia askarijeshi wa kulinda amani wa UNIFIL na kuwauwa.
Nebenzya amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unapasa kuheshimu makubaliano ya usitishaji vita na kufungamana na azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la UN na ametaka kuondoka wanajeshi ghasibu wa Israel katika ardhi ya Lebanon.
Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa pia ametahadharisha kuwa makubaliano yoyote ya amani yataendelea kulegalega iwapo wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel hawataondoka katika ardhi ya Lebanon.