Putin: Washirika wa Ukraine ni washirika wa ugaidi wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i141184-putin_washirika_wa_ukraine_ni_washirika_wa_ugaidi_wa_kimataifa
Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, kurejeshwa uhusiano wa nchi yake na Marekani kunategemea misimamo ya Washington na kusisitiza kwamba: Madola ya Magharibi yanayoshirikiana na Ukraine ni washirika wa ugaidi wa kimataifa.
(last modified 2026-09-04T03:18:21+00:00 )
Sep 04, 2026 03:16 UTC
  • Putin: Washirika wa Ukraine ni washirika wa ugaidi wa kimataifa

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, kurejeshwa uhusiano wa nchi yake na Marekani kunategemea misimamo ya Washington na kusisitiza kwamba: Madola ya Magharibi yanayoshirikiana na Ukraine ni washirika wa ugaidi wa kimataifa.

Shirika la habari la RIA Novosti limemnukuu Rais Vladimir Putin akisema hayo katika hotuba aliyoitoa kwenye "Jukwaa la Uchumi la Mashariki" na kuongeza kuwa: Kuna fursa za kutatua mgogoro wa Ukraine; Russia inazishukuru pande zote zinazojaribu kusaidia kutatua mgogoro wa Ukraine.

Akiendelea na hotuba yake, Putin amesema: China imekuwa ikizingatia kutatua mgogoro wa Ukraine na inaamini kwamba suala hilo linapaswa kutatuliwa kwa njia za amani.

Ameongeza kwamba Washirika wa Ukraine yaani madola ya Magharibi yanayojifanya kukaa kimya ni washirika wa ugaidi wa kimataifa. 

Rais wa Russia amezungumzia pia hali iliyopo katika vita vya Ukraine na kueleza kuwa, kasi ya kusonga mbele jeshi la Russia katika eneo maalumu la operesheni za kijeshi inaongezeka siku baada ya siku. Idadi ya majeruhi wa Ukraine ni kubwa zaidi kuliko idadi ya watu wanaojiunga na vikosi vya jeshi la nchi hiyo kuziba pengo la wanajeshi wanaotoka.  Pia amesema kuwa, lengo la kueneza uvumi kwamba huko Russia kuna uhamasishaji wa watu kujiunga na jeshi ni kujaribu kuvuruga matokeo ya upigaji kura katika uchaguzi ujao nchini humo.

Putin pia amegusia uhusiano wa Russia na Marekani na kusema: Moscow ina marafiki wengi huko Marekani. Russia inataka kurejesha uhusiano kamili na Marekani, lakini hii pia inategemea misimamo ya Washington. Mawasiliano na wawakilishi walioteuliwa na Trump kusimamia mazungumzo baina ya Marekani na Russia bado yapo, na mchakato huo unaendelea.