UN yatahadharisha kuhusu kushindwa kusoma watoto wakimbizi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i15379-un_yatahadharisha_kuhusu_kushindwa_kusoma_watoto_wakimbizi
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetahadharisha kuhusu kushindwa kwenda shule watoto wakimbizi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 15, 2016 11:55 UTC
  • UN yatahadharisha kuhusu kushindwa kusoma watoto wakimbizi

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetahadharisha kuhusu kushindwa kwenda shule watoto wakimbizi.

Filippo Grandi, Mkuu wa shirika la UNHCR ametahadharisha leo katika ripori ya shirika hilo kuhusu kushindwa kupata haki ya msingi ya kusoma watoto wakimbizi na kueleza kuwa watoto hao milioni 3 na laki saba wenye umri wa kwenda shule wanashindwa kwenda shule.

Filippo Grandi Mkuu wa UNHCR

Grandi amesema kuwa suala hilo ni tatizo kwa mamilioni ya watoto wakimbizi na ametoa wito wa kuchukuliwa hatua katika ngazi za kimataifa ili kuwarejesha watoto hao mashuleni. Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, elimu inaweza kuwasaidia wakimbizi kujenga mustakbali wao katika nchi ambazo wamekimbilia au mara watakaporejea makwao.

Filippo Grandi ameyasema hayo kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi na Wahajiri uliopangwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu huko New York, Marekani. Grandi ameongeza kuwa watu milioni 65 na laki tatu duniani wanaishi kama wakimbizi.