Rais Rouhani alakiwa rasmi Vietnam na Rais wa nchi hiyo
Oct 06, 2016 03:56 UTC
Rais wa Vietnam amemlaki rasmi Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko Hanoi mji mkuu wa nchi hiyo.
Hafla ya mapokezi rasmi ya Rais Hassan Rouhani wa Iran imefanyika leo asubuhi katika ikulu ya Rais Tran Dai Quang wa Vietnam. Rais Rouhani na mwenzake wa Vietnam Tran Dai Quang walianza mazungumzo ya pande mbili baada ya mapokezi rasmi ya Rais wa Iran.
Rais Hassan Rouhani pia amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietman Nguyen Xuan PHUC. Rais wa Iran jana alasiri alielekea Hanoi mji mkuu wa Vietnam ikiwa ni kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya kuzitembelea nchi za kusini mashariki mwa Asia.
Tags