Nov 24, 2016 05:25 UTC
  • Mamia waandamana London dhidi ya gazeti la Saudia la Sharq Ausat

Mamia waandamana London dhidi ya gazeti la Saudia la Sharq Ausat Mamia ya watu walifanya maandamano jana mjini London huko Uingereza mbele ya jengo la ofisi za gazeti linalofadhiliwa na Saudi Arabia la al Sharq al Ausat kutokana na kuwavunjia heshima wananchi wa Iraq.

Waandamanaji hao walisema kuwa ripoti ya uongo iliyochapishwa na gazeti hilo dhidi ya Waislamu wa Iraq imeandikwa kwa sababu za kisiasa na chuki za kimadhehebu na kwamba lengo lake ni kuvuruga umoja na mshikamano wa Wairaqi.

Siku chache zilizopiga gazeti la Saudi Arabia la al Sharq al Ausat lilibuni ripoti ya uongo na kuinasibisha kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) ikidai kuwa mamia ya wanawake wa Iraq wanapata uja uzito wa mimba za haramu baada ya shughukli ya kidini ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as) ambayo hufanyika kwa matembezi makubwa ya mamilioni ya Waislamu siku arubaini baada ya terehe 10 Muharram ambayo ndiyo aliyoawa shahidi ndani yake mjukuu huo wa Mtume.

Baada ya kuchapishwa ripoti hiyo Shirika al Afya Duniani (WHO) lilitoa taarifa kali likikadhibisha madai hayo na kusema kuwa litalifungulia mashtaka gazeti hilo la Saudi Arabia kwa kuandika habari ya uongo.

Saudi Arabia na washirika wake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali hususan vyombo vya habari kuchochea fitina na hitilafu za kimadhehebu kati ya Waislamu. Nchi hiyo ya kifalme pia inayaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kigaidi yanayowakufurusha Waislamu wengine kama Daesh ambayo yanafanya mauaji ya kutisha katika nchi kama Iraq na Syria.  

Tags