Mkuu wa Waislamau Ujerumaini atumiwa mamia ya ujumbe wa vitisho
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24139-mkuu_wa_waislamau_ujerumaini_atumiwa_mamia_ya_ujumbe_wa_vitisho
Mkuu wa jamii ya Waislamu nchini Ujerumaini amesema kuwa, ametumiwa mamia ya ujumbe wa vitisho unaotishia kumuua na kumkatishia maisha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 23, 2017 23:27 UTC
  • Mkuu wa Waislamau Ujerumaini atumiwa mamia ya ujumbe wa vitisho

Mkuu wa jamii ya Waislamu nchini Ujerumaini amesema kuwa, ametumiwa mamia ya ujumbe wa vitisho unaotishia kumuua na kumkatishia maisha.

Shirika la habari la Fars limemnukuu Aiman Mazyek, mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumaini akisema hayo Jumatatu na kuongeza kwamba, ujumbe huo wa vitisho ametumiwa kwa njia ya B-pepe na mtandao wa kijamii wa Facebook.

Mkuu huyo wa jamii ya Waislamu wa Ujerumaini ameongeza kuwa, kila siku anatumiwa mamia ya ujumbe wa vitisho kwa njia tofauti.

Aiman Mazyek, mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Ujerumaini

 

Amesema, vitisho na vitendo vya kushambuliwa Waislamu viliongezeka maradufu mwaka 2015 na mambo yote hayo wameyaripoti kwa vyombo vya mahakama vya Ujerumaini.

Vitisho na vitendo vya kushambuliwa Waislamu barani Ulaya ikiwemo Ujerumaini vimeongezeka sana katika miezi ya hivi karibuni.

Genge lenye chuki za kidini na lililo dhidi ya Uislamu lijulikanalo kwa jina la Pegida limefanya mashambulizi kadhaa dhidi ya Waislamu huko Ujerumaini.