Ujerumani yakosoa sheria ya kibaguzi ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24437-ujerumani_yakosoa_sheria_ya_kibaguzi_ya_marekani
Kansela wa Ujerumani amekosoa hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kupasisha sheria ya kuwazuia wakimbizi na raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia Marekani.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 30, 2017 01:10 UTC
  • Ujerumani yakosoa sheria ya kibaguzi ya Marekani

Kansela wa Ujerumani amekosoa hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump kupasisha sheria ya kuwazuia wakimbizi na raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia Marekani.

Angela Merkel, Kansela wa Ujeruamani amesema jitihada za kimataifa za kupambana na ugaidi hazifai kutumiwa kama kisingizio cha kuhalalisha sheria hiyo ya kibaguzi.

Merkel ameyasema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Trump na kumkumbusha rais huyo mpya wa Marekani kuhusu umuhimu wa kuheshimiwa Mkataba wa Geneva, unaoitaka jamii ya kimataifa kuheshimu haki za wakimbizi katika misingi ya ubinadamu. 

Trump akisaini sheria ya kutoruhusiwa Marekani wakimbizi wa nchi za Kiislamu

Naye  Steffen Seibert, msemaji wa Kansela wa Ujerumani amesema kuwa, kupambana na ugaidi hakuipi nchi yeyote sababu ya kumshuku na kumbagua mtu kwa misingi ya imani yake ya kiroho.

Wakati huohuo, chama cha Green Party cha Ujerumani kimekosoa sheria hiyo ya kibaguzi ya Marekani na kubainisha kuwa, Donald Trump sio mshirika wa kutegemewa tena na Ujerumani.

Ijumaa iliyopita, Trump ilipasisha sheria ya kutoruhusiwa nchini Marekani kwa muda wa miezi mitatu wakimbizi na watu kutoka nchi zenye idadi kubwa ya Waislamu, ambazo ni Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen, kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.