Russia yasisitiza kutekelezwa makubaliano ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24961-russia_yasisitiza_kutekelezwa_makubaliano_ya_jcpoa
Balozi wa Russia nchini Marekani amesisitiza udharura wa kutekeleza makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la nchi 5+1 na Iran yaani JCPOA.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 10, 2017 11:51 UTC
  • Russia yasisitiza kutekelezwa makubaliano ya JCPOA

Balozi wa Russia nchini Marekani amesisitiza udharura wa kutekeleza makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la nchi 5+1 na Iran yaani JCPOA.

Sergey Kislyak amesema kuwa makubaliano ya JCPOA yamekamilika na kwamba hitilafu zilizopo kati ya Moscow na Washington kuhusu Iran zaidi zinahusiana na lugha iliyotumiwa na si kuhusu asili ya makubaliano hayo. Kislyak amesema pia kwamba makubaliano ya JCPOA ni makubaliano yenye taathira na yanayotekelezwa na kuongeza kuwa, anataraji kuwa makubaliano hayo yataendelea kutekelezwa katika duru ya uongozi wa serikali mpya ya Marekani.

Balozi wa Russia nchini Marekani ametahadharisha pia kuhusu hatua yoyote ya kufuta au kukwamishwa JCPOA na kueleza kuwa, hatua kama hizo siku zote huwa na taathira hasi. 

Kamisheni ya JCPOA ikijadili maudhui za utekelezaji 

Uungaji mkono wa nchi za Ulaya kwa makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 ni hatua nyingine inayothibitisha kwamba Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo vinaamini Iran imetekeleza ahadi zake zote kuhusu JCPOA.

Hata hivyo Rais Mpya wa Marekani anayezusha makelele na mivutano wa Marekani, Donald Trump hivi karibuni alisisitiza kwa mara nyingine kwamba ataendeleza siasa zake za uhasama dhidi ya Iran na kusema kuwa makubaliano ya JCPOA ni makubaliano mabaya zaidi kuwahi kufikiwa hadi sasa.