Barret: Matamshi ya Trump dhidi ya Iran, dhihirisho kuwa ni punguani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i25212-barret_matamshi_ya_trump_dhidi_ya_iran_dhihirisho_kuwa_ni_punguani
Mchanganuzi wa masuala ya siasa na mwandishi wa habari wa Marekani amesema matamshi ya kukinzana yanayotolewa mara kwa mara na Rais wa Marekani Donald Trump na hususan matamshi aliyoyatoa hivi karibuni dhidi ya Iran yanadhihirisha kuwa bilionea huyo ana matatizo ya kiakili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 16, 2017 04:03 UTC
  • Barret: Matamshi ya Trump dhidi ya Iran, dhihirisho kuwa ni punguani

Mchanganuzi wa masuala ya siasa na mwandishi wa habari wa Marekani amesema matamshi ya kukinzana yanayotolewa mara kwa mara na Rais wa Marekani Donald Trump na hususan matamshi aliyoyatoa hivi karibuni dhidi ya Iran yanadhihirisha kuwa bilionea huyo ana matatizo ya kiakili.

Kevin Barrett aliyasema hayo jana katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Press TV na kubainisha kuwa, kauli ya Trump baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran kwa mara nyingine tena imeudhihirishia ulimwengu kuwa Marekani inaongozwa na rais mwenye matatizo makubwa ya kisaokolijia.

Katika kikao na waandishi wa habari pambizoni mwa Netanyahu katika Ikulu ya White House, Trump alisema Washington itatumia kila njia kuhakikisha kuwa Iran haitengezi silaha za nyuklia.

Kevin Barret, mchambuzi wa siasa wa Marekani

Hii ni katika hali ambayo, mbali na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, idara za ujasusi za Marekani na Israel zimekuwa zikikariri kuwa, mradi wa nyuklia wa Iran ni wa malengo ya amani.

Kevin Barret amesisitiza kuwa, nchini Marekani mijadala na minong'ono inaendelea kufanyika katika kona mbali mbali za nchi kuhusu hali ya kiafya ya Trump, baadhi ya wanasaikolijia wakisema kuwa rais huyo wa Marekani anahitaji matibabu ya haraka kabla ya mambo kuharibika zaidi. 

Mchanganuzi huyo wa masuala ya kisiasa wa Marekani amesema Netanyahu anatumia fursa hiyo ya matatizo ya kisaikolojia ya trump, kumshinikiza aitumbukize Marekani vitani na Iran.