Sayyed Albeity wa Lamu, Kenya: Kuna Matumaini Intifadha ya Palestina Itafaulu
(last modified Sun, 26 Feb 2017 14:50:08 GMT )
Feb 26, 2017 14:50 UTC

Mkutano wa Sita wa Kimataifa wa Kuunga Mkono Intifadha ya Palestina ulimalizika Jumatano hapa Tehran, ambapo kulikuwa wa washiriki zaidi ya 700 kutoka 80.

Mkutano ulimalizika kwa kusisitizia udharura wa kulindwa kadhia ya Palestina ambayo ni kipaumbele cha kwanza cha nchi ulimwengu wa Kiislamu na za Kiarabu na ndilo zingatio kuu la fikra za walio wengi duniani.

Kati ya walioshiriki katika mkutano huo alikuwa ni Sayyed Hassan Albeity mwanasiasa mwandamizi wa Kaunti ya Lamu nchini Kenya ambaye alizungumza na mwandishi wa Radio Tehran Mubarak Henia baada ya mkutano na ana matumaini kuwa Wapalestina watafanikiwa katika mwamako wao wa kujikomboa kutoka makucha ya utawala ghasibu wa Israel. Sikiliza mahojiano kupata tathmini yake kamili ya mkutano huo