Chuki zaongezeka Marekani baada ya kuchaguliwa Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i26184-chuki_zaongezeka_marekani_baada_ya_kuchaguliwa_trump
Wamarekani waliowengi wanaamini kuwa kiwango cha chuki kimeongezeka nchini humo baada ya kuchaguliwa Donald Trump kama rais.
(last modified 2026-04-28T05:09:17+00:00 )
Mar 10, 2017 04:09 UTC
  • Chuki zaongezeka Marekani baada ya kuchaguliwa Trump

Wamarekani waliowengi wanaamini kuwa kiwango cha chuki kimeongezeka nchini humo baada ya kuchaguliwa Donald Trump kama rais.

Asilimia 63 ya wapiga kura Marekani wanasema kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la chuki na taasubi tokea Trump achaguliwe Novemba 2016 huku asilimia 32 wakiamini kuwa hakuna chochote kilichobadilika.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Quinnipiac huko Connecticut, asilimia 77 ya Wamarekani wanaamini kuwa watu wa jamii za waliowachache wanaonewa na kudhulumiwa.

Bango la kupinga ujenzi wa misikiti Marekani

Takwimu zinaonesha kuwa uhalifu unaosababishwa na chuki hususan dhidi ya Waislamu umeongezeka nchini Marekani tangu Donald Trump achaguliwe kuongoza nchi hiyo.

Wataalamu wanasisitiza kuwa, matamshi ya kibaguzi ya Trump pamoja na sera zake ni chanzo cha chuki, mashambulizi na hujuma zinazofanywa na makundi ya kibaguzi dhidi ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani.