Sanders: Trump ataitumbukiza Marekani katika utawala wa kiimla
https://parstoday.ir/sw/news/world-i26274-sanders_trump_ataitumbukiza_marekani_katika_utawala_wa_kiimla
Aliyekuwa mgombea tiketi ya kukiwakilisha chama cha Democrati katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka jana 2016, Bernie Sanders ameonya kuwa Rais Donald Trump ataitumbukiza nchi hiyo katika utawala wa kidikteta na kiimla.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 12, 2017 04:22 UTC
  • Sanders: Trump ataitumbukiza Marekani katika utawala wa kiimla

Aliyekuwa mgombea tiketi ya kukiwakilisha chama cha Democrati katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka jana 2016, Bernie Sanders ameonya kuwa Rais Donald Trump ataitumbukiza nchi hiyo katika utawala wa kidikteta na kiimla.

Sanders ambaye ni Seneta wa Jimbo la Vermont amesema sera za Trump zinaonyesha wazi kuwa bilionea huyo anaelekea kuitumbukiza Marekani katika utawala wa kimabavu.

Mwanasiasa huyo ambaye alichuana na Hillary Clinton kuwania nafasi ya mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic mwaka jana amebainisha kuwa, Trump amekuwa akikiuka wazi wazi katiba ya nchi, jambo ambalo linadhihirisha kuwa ni kiongozi dikteta.

Rais Trump wa Marekani

Bernie Sanders kadhalika amesema kuwa: "Trump ni mtu mrongo, anawadanganya Wamarekani wakati wote, sio kwa bahati mbaya, anafanya hivyo makusudi ili kukanyaga misingi ya demokrasia."

Amesema mienendo hiyo ya kidikteta na urongo pamoja na sera mbovu za kiuchumi vimewasukuma Wamarekani wafanye maandamano kila uchao kukosoa utawala wake.

Kadhalika mwanasiasa huyo mkongwe wa Marekani amekosoa tabia ya Trump ya kutumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa dikrii zisizo na mantiki pasina kutafuta ushauri wa kisheria au miongozo ya katiba.