Maandamano makubwa dhidi ya Trump, Wamarekani 39 wauawa na kujeruhiwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i28138-maandamano_makubwa_dhidi_ya_trump_wamarekani_39_wauawa_na_kujeruhiwa
Zaidi ya Wamarekani 40 elfu wakiwemo wasomi na wataalamu mashuhuri wa nchi hiyo wameshiriki kwenye maandamano mjini Washington ya kumpinga Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kulalamikia sera zake za mazingira.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Apr 23, 2017 03:17 UTC
  • Maandamano makubwa dhidi ya Trump, Wamarekani 39 wauawa na kujeruhiwa

Zaidi ya Wamarekani 40 elfu wakiwemo wasomi na wataalamu mashuhuri wa nchi hiyo wameshiriki kwenye maandamano mjini Washington ya kumpinga Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kulalamikia sera zake za mazingira.

Shirika la habari la IRIB limeripoti kuwa, waandamanaji wamekusanyika mbele ya Ikulu ya Marekani White House na mbele ya majengo ya Congress na Wizara ya Mazingira mjini Washington.

Maandamano hayo yamefanyika huku kikao cha kila mwaka cha Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kikiendelea mjini Washington. Waandamanaji walipiga nara wakimtaka Trump apunguze kuvamia nchi nyingine na ashughulikie masuala ya masomo na malezi. Vile vile wamemwita Trump kuwa ni fashisti na kulaani siasa za kupenda vita za Marekani.

Mauaji na vitendo vya kikatili ni mambo ya kila siku nchini Marekani

 

Katika upande mwingine, Wamarekani wasiopungua saba wameuawa kwa kupigwa risasi na 32 wengine wamejeruhiwa katika matukio 52 ya kupigana risasi yaliyotokea katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kwenye maeneo tofauti ya Marekani.

Kituo cha kukusanya taarifa za matumizi ya silaha nchini Marekani kimetangaza kuwa, baadhi ya matukio hayo yametokea Chicago, mji mkubwa zaidi ya jimbo la Illinois na vile vile katika majimbo la California, New Jersey na majimbo mengine ya Marekani. 

Kwa mujibu wa kituo hicho, watu 39 wameuawa na 82 wengine wamejeruhiwa kwa risasi katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita kwenye majimbo mbalimbali ya Marekani.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2017 hadi hivi sasa, matukio elfu 13 na 154 ya kupigana risasi yameripotiwa katika miji tofauti ya Marekani na kiujumla watu elfu tatu na 354 wameuawa na elfu sita na 353 wengine wamejeruhiwa katika kipindi hicho.