Hizbullah yasisitizia umoja wa Waislamu dhidi ya adui Mzayuni
Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon, Sheikh Naim Qassem amesisitizia umuhimu wa kuendelezwa mapambano dhidi ya adui Mzayuni.
Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo kupitia mazungumzo ya simu na Sheikh Ibrahim al-Sunusi, Katibu Mkuu wa chama cha Kongresi ya Wananchi nchini Sudan ambapo sanjari na kukumbusha umuhimu na udharura wa kuimarishwa umoja baina ya Waislamu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hususan za adui Mzayuni, ametaka pia kuendelezwa ushirikiano kati ya harakati ya Hizbullah na Kongresi ya Wananchi nchini Sudan. Sheikh Qassem pia akimwakisha Katibu Mkuu wa Hizbullah, Hassan Nasrallah ametoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Sheikh Hassan Al-Turabi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Kongresi ya Wananchi nchini Sudan.
Itafahamika kuwa, baada ya kufariki dunia Sheikh Hassan Al-Turabi, shakhsia wa kisiasa na kitamaduni nchini Sudan, wafuasi wa chama cha Kongresi ya Wananchi nchini Sudan wamemteua Ibrahim al-Sunusi kuwa katibu mkuu chama hicho.