Mogherini: EU na Russia zina msimamo mmoja kuhusu JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29120-mogherini_eu_na_russia_zina_msimamo_mmoja_kuhusu_jcpoa
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema EU na Russia zina msimamo mmoja katika kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 15, 2017 03:26 UTC
  • Mogherini: EU na Russia zina msimamo mmoja kuhusu JCPOA

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema EU na Russia zina msimamo mmoja katika kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Shirika la habari la IRNA limenukuu Mogherini akisema kuwa, kuna baadhi ya mafaili ya makubaliano hayo yaliyofikiwa Julai mwaka 2015 ambayo kwayo Umoja wa Ulaya na Russia zinayatizama kwa jicho moja.

Sisitizo hilo la Mogherini limetokana na wasiwasi wa EU juu ya kukiukwa makubaliano hayo na Rais wa Marekani Donald Trump.

Makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayofahamika kama JCPOA

Katika kampeni za uchaguzi wa rais, Trump aliahidi kuyachana makubaliano hayo ya Vienna katika siku zake za kwanza uongozini.

Kadhalika Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa, msimamo wa EU na Russia katika mgogoro wa Palestina na Israel unaoana.

Hata hivyo hakufafanua zaidi kuhusu msimamo huo, lakini mara kwa mara Umoja wa Ulaya umekuwa ukikosoa kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.