Mogherini: Marekani itafungamana na mapatano ya nyuklia ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i30412-mogherini_marekani_itafungamana_na_mapatano_ya_nyuklia_ya_iran
Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya amesema pamoja na kuwepo malalamiko ya serikali ya Marekani kwa mapatano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1, ana matumaini kuwa Washington itayatekeleza kwani ni ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2017 08:53 UTC
  • Mogherini: Marekani itafungamana na mapatano ya nyuklia ya Iran

Mkuu wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya amesema pamoja na kuwepo malalamiko ya serikali ya Marekani kwa mapatano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1, ana matumaini kuwa Washington itayatekeleza kwani ni ya kimataifa.

Federica Mogherini Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya ameyasema hayo Jumanne katika Mkutano wa Kimataifa wa Amani wa Oslo na kuongeza kuwa, hatua ya Marekani ya kuyatathmini upya mapatano hayo itapelekea wakuu wa Washington wafikie natija ya kimantiki nayo ni kuyalinda mapatano hayo.

Mogherini pia ameafikiana na kauli ya Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye alisema Iran inafungamana na mapatano ya nyuklia.

Mawaziri wa Kigeni wa 5+1, mkuu wa sera za kigeni wa EU na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran baada ya mapatano ya JCPOA Julai 2015

Ameongeza dhana zote mbaya kuhusu mapatano hayo zimetoweka hasa kwa kuzingatia ripoti ya jana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kuhusu kufungamana Iran na mapatano hayo ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA. Mapatano hayo sasa yanakaribia mwaka wa pili tokea yatiwe saini.

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema JCPOA si mapatano ya nchi moja bali ni mapatano ya kimataifa na kwamba EU itahakikisha yanatekelezwa.

Mkutano wa Amani wa Oslo umeanza Jumanne katika mji mkuu wa Norway kwa kuhudhuriwa na Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka pembe mbali mbali za dunia.