Rais wa Ufaransa awapongeza Waislamu kwa kupambana na ugaidi, misimamo mikali
https://parstoday.ir/sw/news/world-i30780-rais_wa_ufaransa_awapongeza_waislamu_kwa_kupambana_na_ugaidi_misimamo_mikali
Raisi mpya wa Ufaransa ameipongeza jamii ya Waislamu wa nchi hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kupambana na misimamo mikali na amesisitiza udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya ugaidi.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Jun 21, 2017 09:35 UTC
  • Rais wa Ufaransa awapongeza Waislamu kwa kupambana na ugaidi, misimamo mikali

Raisi mpya wa Ufaransa ameipongeza jamii ya Waislamu wa nchi hiyo kutokana na mchango wake mkubwa katika kupambana na misimamo mikali na amesisitiza udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya ugaidi.

Emmanuel Macron ambaye ameshiriki katika dhifa ya chakula cha futari iliyotayarishwa na Baraza la Waislamu wa nchi hiyo, ametilia mkazo sana suala la kupambana na ugaidi na harakati za kueneza misimamo mikali. 

Amesema kuwa, mapambano dhidi ya ugaidi wa zama hizi mbali na vikosi vya usalama, yanahitajia jibu la kimaadili na kiutamaduni la makundi yote.

Waislamu wa Ufaransa

Rais wa Ufaransa amepongeza misimamo ya Baraza la Waislamu wa Ufaransa kuhusu mashambulizi ya kigaidi yaliyoilenga nchi hiyo katika miaka ya hivi karibuni na kusema: Watu wote duniani wanapaswa kupambana na mitazamo isiyo sahihi inayokusudia kuchafua sura ya Uislamu. 

Emmanuel Macron amesisitiza kuwa, hakuna mtu anayeweza kudai kuwa itikadi za kidini za Waislamu hazioani na sheria na wala hakuna mtu anayeweza kuwataka Wafaransa wasiheshimu sheria.