Lavrov akosoa harakati za Marekani dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i30854-lavrov_akosoa_harakati_za_marekani_dhidi_ya_russia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekosoa hatua ya Marekani ya kuiwekea nchi yake vikwazo vipya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 23, 2017 03:34 UTC
  • Lavrov akosoa harakati za Marekani dhidi ya Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amekosoa hatua ya Marekani ya kuiwekea nchi yake vikwazo vipya.

Sergei Lavrov amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuhusu hitilafu zilizopo kati ya nchi mbili hizo na pande hizo zimedilishana mawazo kuhusu hali ya mambo huko Syria na mgogoro wa Ukraine. 

Lavrov pia amekemea vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya nchi yake akisema vinawekwa kwa ajili ya kuishinikiza Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameashiria pia harakati za muungano unaoongozwa na Marekani huko Syria na kusisitiza kuwa, hatua za aina hiyo zinakiuka haki ya kujitawala nchi ya Syria na kutatiza mapambano ya kuwaangamiza magaidi na kutafuta ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo. 

Magaidi wa Daesh wanaozusha hali ya mchafukoge huko Syria  

Serikali ya Marekani Jumanne wiki hii iliendeleza vikwazo vyake dhidi ya Russia ambapo iliwawekea vikwazo shakhsia 38 na makampuni ya Russia  na  raia wa Ukraine wanaoipinga serikali ya Kiev kuhusiana na hitilafu za miaka kadhaa kuhusu eneo la Crimea.