Jul 04, 2017 15:42 UTC
  • Waislamu Marekani wakumbuka uhalifu wa mawahabi wa kubomoa makaburi ya Maswahaba

Waislamu katika maeneo mbalimbali wamekusanyika wakikumbuka kitendo kiuvu cha kubomolewa makaburi ya Jannat al-Baqi'i mjini Madina kilichofanywa na mawahabi wa Saudi Arabia miongo kadhaa iliyopita.

Maandamano kama hayo ya kuonesha hasira za Waislamu na kukumbuka tukio hilo chungu yamefanyika mjini Washington, Marekani ambapo waandamanaji wamepinga fikra na itikadi za kuchupa mipaka za kiwahabi ambazo ndiyo chimbuko la kundi la kitakfiri la Daesh linaloendelea kuua watu hususan Waislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Waandamanaji hao walibeba mabango yenye maandishi: "Uwahabi upingwe marufuku", "simamisheni ugaidi wa kiwahabi", "Waislamu dhidi ya genge la ISIS" na "ISIS ni Uwahabi".

Vilevile wametoa wito wa kujengwa upya minara na maziara ya Jannat al-Baqi'i yenye makaburi ya wajukuu, wake na masahaba wa Mtume wetu Muhammad (saw).

Waislamu wakitaka Baqi'i ijengwe upya

Tarehe 8 Shawwal mwaka 1345 Hijria (miaka 92 iliyopita) mawahabi wanaotawala Saudi Arabia walivamia makaburi ya Baqi'i katika mji mtakatifu wa Madina na kuvunja turathi za Kiislamu na makaburi ya watu wa familia ya Mtume Muhammad (saw) yakiwemo makaburi ya mjuu wake Imam Hassan bin Ali, mama aliyemlea Fatima binti Assad, ami yake Abbas na masahaba wake wengi.

Makaburi ya Baqi'i kwa sasa baada ya kubomolewa

Mwenendo huo huo unaendelezwa na mawahabi wa Saudia na vikaragosi vyao yaani Daesh, Boko Haram na al Shabab katika maeneo mbalimbali duniani.

Tags