Jul 12, 2017 08:12 UTC
  • Mtafiti wa Kiirani aliyekuwa anashikiliwa Marekani aachiliwa huru

Mtafiti wa Kiirani wa masuala ya kensa aliyekamatwa hivi karibuni mara tu baada ya kuwasili Marekani ameachiliwa huru na kurudishwa humu nchini.

Muhsen Dehnavi mtafiti wa masuala ya saratani wa Iran ambaye siku ya Jumatatu alikamatwa na kuzuiliwa katika uwanja wa ndege wa Logan katika jimbo la Boston mara tu baada ya kuwasili nchini Marekani akiwa ameandamana na mkewe pamoja na mtoto wao alirejea hapa nchini siku ya Jumanne. Mtafiti huyo mtajika wa Iran alikuwa katika safari ya kikazi ambapo alikuwa amealikwa kufundisha katika mojawapo ya vyuo mashuhuri vya Boston ambacho kiko chini ya usimamizi wa Chuo cha Tiba cha Harvard. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chuo hicho cha hospitali ya watoto ya Boston, kutiwa mbaroni mtaalamu huyo wa Kiirani kidhahiri hakuhusiani na amri iliyotolewa hivi karibuni na Rais Donald Trump wa Marekani ambayo inapiga marufuku raia wa nchi sita za Kiislamu ikiwemo Iran, kusafiri Marekani, kwa sababu msomi huyo alikuwa na kibali halali cha kuingia nchini humo.

Visa ya Marekani

Kwa mujibu wa Susan Church, mkuu wa kituo cha mawakili wanaoshughulikia masuala ya wahamiaji katika eneo la New England nchini Marekani amesema kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, huenda hatua ya kukamatwa Dehnavi na familia yake ikawa ni ya kipumbavu zaidi kuliko ya kuzuiwa kuingia Marekani kwa sababu sheria za nchi hiyo zinasema wazi kuwa mtu aliye na kibali halali cha kuingia nchini Marekani anapasa kuruhusiwa kufanya hivyo.

Tags