Congress ya Marekani yataka kufanyike mazungumzo na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i31796-congress_ya_marekani_yataka_kufanyike_mazungumzo_na_iran
Congress imepasisha mswada ambao unailazimisha Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo yaani Pentagon kutafuta njia za kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuepuka makabiliano ya kijeshi katika maji ya Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2017 03:21 UTC
  • Congress ya Marekani yataka kufanyike mazungumzo na Iran

Congress imepasisha mswada ambao unailazimisha Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo yaani Pentagon kutafuta njia za kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuepuka makabiliano ya kijeshi katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

Marekebisho yaliyofanyiwa mswada huo unaojulikana  kama National Defense Authorization Act, ambayo yaliyowasilishwa bungeni na John Canaries na Robben Gallo wabunge wa chama cha  Democrats yalipasishwa siku ya Alkhamisi bila ya pingamizi. Kwa mujibu wa mswada huo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon, imetakiwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje kwa madhumuni ya kuwasilisha ripoti kuhusiana na uwezekano wa kufanyika mazungumzo na Iran kwa lengo la kuepuka makabiliano ya kijeshi baharini.

Congress ya Marekani

Kwa mujibu wa marekebisho yaliyofanyiwa mswada huo, Wizara ya Ulinzi kwa ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inatakiwa kuwasilisha ripoti kwa kamati za Congress kuhusiana na faida za kuwepo mazungumzo ya pande mbili au pande kadhaa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi nyingine za eneo la Ghuba ya Uajemi ili kuepusha makabiliano yaliyotajwa. Lengo la kuwasilishwa mswaada huo ni kuepusha makabiliano ya baharini katika Ghuba ya Uajemi na lango la bahari la Hormoz. Hata hivyo mswada huo unapaswa kuwasilishwa kwa Seneti ya Marekani ili upasishwe kuwa sheria. Wakati huohuo Baraza la Kitaifa la Wairani na Wamarekani, limekaribisha mswada huo na kusema ni ushindi kwa wanaounga mkono udipomasia kwa madhumuni ya kuepusha makabiliano ya kijeshi kati ya Iran na Marekani.