Jarida la Stern: Mamia ya watoto wamenajisiwa katika Kanisa Katoliki Ujerumani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i31964-jarida_la_stern_mamia_ya_watoto_wamenajisiwa_katika_kanisa_katoliki_ujerumani
Jarida moja la kila wiki la Ujerumani limechapisha uchunguzi uliofanywa na mwanasheria wa nchi hiyo ambao umebaini kuwa, watoto 547 wa kundi la kwaya katika Kanisa Kuu la Dayosisi la Katoliki nchini Ujerumani, wamenajisiwa.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 19, 2017 02:29 UTC
  • Jarida la Stern: Mamia ya watoto wamenajisiwa katika Kanisa Katoliki Ujerumani

Jarida moja la kila wiki la Ujerumani limechapisha uchunguzi uliofanywa na mwanasheria wa nchi hiyo ambao umebaini kuwa, watoto 547 wa kundi la kwaya katika Kanisa Kuu la Dayosisi la Katoliki nchini Ujerumani, wamenajisiwa.

Jarida la kila wiki la Stern limemnukuu mwanasheria Ulrich Weber akisema kuwa, vitendo vya kunajisiwa watoto wadogo vinafanyika katika shule za chekechea na sekondari zinazosimamiwa na Kanisa Kuu la Dayosisi la Katoliki nchini Ujerumani. 

Ulrich Weber ameongeza kuwa, watu 49 waliohusika na uhalifu huo wamejulikana.

Habari hiyo imechapishwa baada ya kufichuliwa kashfa nyingi za kunajisiwa watoto wadogo katika shule zinazosimamiwa na Kanisa Katoliki kwa miaka mingi katika nchi mbalimbali za Magharibi. Suala hilo limetoa changamoto kubwa kwa viongozi wa kanisa hilo huko Vatican. Viongozi wa ngazi za juu wa kanisa hilo wanalaumiwa kuwa wamekuwa wakificha kesi za vitendo viovu vya kunajisiwa watoto vinavyofanywa na makasisi na mapadre na kuwakingia kifua wale wanaopatikana na kesi hizo.