Waislamu wakumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume, Imam Sadiq (as)
(last modified Thu, 20 Jul 2017 04:51:35 GMT )
Jul 20, 2017 04:51 UTC
  • Waislamu wakumbuka mauaji ya mjukuu wa Mtume, Imam Sadiq (as)

Waislamu kote duniani hususan wafuasi na wapenzi wa Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saw) leo tarehe 25 Mfunguo Mosi Shawwali wanakumbuka na kuombeleza tukio chungu la kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume huyo wa Mwenyezi Mungu, Imam Ja'far Sadiq (as).

Shughuli ya kukumbuka tukio la kuhuzunisah la kuuawa shahidi Imam Sadiq zimefanyika na zinaendelea katika nchi nyingi duniani ambako wafuasi na wapenzi wa Ahlibaiti wa Mtume tangu jana usiku walikusanyika katika misikiti, maeneo ya ibada ya kumbi mbalimbali za mausuala ya kijamii wakiomboleza na kumuenzi mjukuu huyo wa Mtume (saw). 

Hapa nchini Iran shughuli hizo za kukumbuka tukio la kuuliwa shahidi Imam Ja'far Sadiq (as) zilizoanza jana zinaendelea kote nchini husuan katika miji mitakatifu ya Qum na Mash'had. 

Imam Ja'far Sadiq ambaye ni miongoni wa wajukuu wa Mtume Mtukufu amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na Ali zake, aliuawa shahidi kwa amri ya mtawala dhalimu wa Kiabbasi Mansur al Dawaniqi.

Makaburi ya wajukuu wa Mtume Muhammad (saw) Baqi mjini Madina baada ya kubomolewa na Mawahabi wa Saudia

Alishika hatamu za kuongoza Umma wa Kiislamu akiwa na umri wa miaka 31 baada ya kuuawa shahidi baba yake, Imam Muhammad Baqir. Imam Sadiq ambaye kipindi cha uongozi wake kilisadifiana na zama za mapigano makali kati ya watawala wa Kiumawi na Kiabbasi, alitumia fursa hiyo kueneza elimu na maarifa sahihi ya Kiislamu. Alifanikiwa kulea na kutayarisha wasomi hodari katika taaluma mbalimbali kama tiba, kemia, hesabati, nujumu hadithi na kadhalika. Jabiri bin Hayyan ambaye anatambuliwa hii leo kuwa ndiye baba wa elimu ya kemia alikuwa mwanafunzi wa Imam Ja'far Sadiq (as). 

Tags