Mashambulizi ya kigaidi ya Uhispania
https://parstoday.ir/sw/news/world-i33304-mashambulizi_ya_kigaidi_ya_uhispania
Shambulizi la kigaidi lililotokea jana katika mji wa Barcelona nchini Uhispania limezusha wahka na wasiwasi mkubwa katika mji huo na miji mingine ya nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 18, 2017 08:41 UTC
  • Mashambulizi ya kigaidi ya Uhispania

Shambulizi la kigaidi lililotokea jana katika mji wa Barcelona nchini Uhispania limezusha wahka na wasiwasi mkubwa katika mji huo na miji mingine ya nchi hiyo.

Polisi ya jimbo la Catalonia na Waziri wa Mambo ya Ndani wa eno hilo wamethibitisha kuwa watu 13 wamefaiki dunia katika hujuma hiyo na wengine 100 wamerehiwa. Hali ya majeruhi 15 miongoni mwao imeripotiwa kuwa ni mbaya sana na kuna uwezekani idadi ya watu waliouawa ikaongezeka. 

Alasiri ya jana gari dogo iliingia ghafla katika eneo la wapita njia katika eneo la kitalii la Las Ramblas katikati ya jiji la Barcelona na kukanyaga makumi ya watu waliokuwa wakitembea kwa miguu. Eneo hilo limejaa maduka na vituo vya kibiashara. Mitaa ya eneo la Las Ramblas imejengwa kwa namna ambayo wapita njia na watu wanaotembea kwa miguu hupita katikati na magari yanapita pande mbili za kulia na kushoto. Maafisa wa Uhispania wanataja sambulizi hilo kuwa na la kigaidi. Masaa machache baadaye kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa ndilo lililofanya shambulizi hilo.

Mapema leo Ijumaa pia polisi ya Uhispania imewapiga risasi na kuwaua watu watano wanaoshukiwa kuwa magaidi. Watu hao walijaribu kugonga watu waliokuwa wakitembea kwa miguu katika eneo la Cambrils lililoko umbali wa kilomita 120 kutoka Barcelona. Polisi wanasema washukiwa hao wamejeruhi raia 6 na polisi mmoja. Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo la Catalonia, Joaquim Forn amesema, kuna uwezekano wa kuwepo mfungamano baina ya mashambulizi hayo mawili.

Shambulizi la kigaidi Barcelona

Kabla ya Uhispania magaidi wa kundi la Daesh waliwahi kutumia mbinu hiyo ya kuua na kujeruhi raia wa kawaida wanaotembea kwa miguu kwa kuwagonga kwa magari katika nchi za Ufaransa, Ujerumani na Italia. Katika mbinu hiyo mpya magaidi hao wanatumia njia za mauaji ambazo ni vigumu sana kuweza kuzitazamia na kuzizuia.

Mashambulizi ya Catalonia huko Uhispania yamedhihirisha tena kwamba, si rahisi kukabiliana na ugaidi kwa kuchukua hatua kali za kiusalama peke yake. Mashambulizi haya pia yanasisitiza uharura wa nchi za Ulaya na Magharibi kwa ujuma kuacha misimao ya kindumakuwili kuhusu ugaidi. Huwezi kuwa na uhusiano wa kistratijia na watawala kama wa Saudi Arabia ambao ndio wafadhili na waungaji mkono wakubwa wa makundi ya kigaidi na utawala ambao ndiyo chimbuko na makao makuu ya fikra za kitakfiri na kiwahabi zinazowakufurisha Waislamu wengine na kuhalalisha damu za wasiokuwa wao, na wakati huo huo utarajie kwamba nchi za Ulaya zitasalimika na mashambulizi ya kigaidi. 

Magaidi wa Daesh wanafadhiliwa na kuungwa mkono na Saudi Arabia

Hii leo kila siku raia elfu tano wa Yemen wengi wao wakiwa watoto wanapatwa na maradhi ya kipindupindu kutokana na mashambulizi na mzigiro wa Saudia na waitifaki wake wa nchi za Magharibi dhidi ya taifa la Yemen. Umoja wa Mataifa umeitangaza Saudi Arabia kuwa ndiye mhusika mkuu wa maafa yanayowapata watu wa Yemen wanaoendelea kupoteza maisha kila siku lakini hakuna nchi hata moja ya Magharibi iliyochukua hatua ya maana dhidi ya Saudi Arabia, na badala yake zinaendelea kuupigia makofi na kuuunga mkono utawala wa kifame wa Aal Saud kwa kuuzia silaha zaidi.

Mfalme Salman wa Saudia na Donald Trump

Sambamba na mashambulizi hayo ya Barcelona kumetokea mashambulizi mengine kama hayo Nigeria, Afghanistan, Syria na Iraq lakini hakuna nchi hata moja ya Magharibi iliyochukua msimamo mkali na kukemea mashambulizi hayo.

Baada tu ya shambulizi la Las Ramblas huko Barcelona kumetokea wimbi kubwa la sauti za serikali na viongozi wa nchi za Magharibi wakilaani hujuma hiyo ya kigaidi. Hili ni jibu na msimamo sahihi wa kibinadamu, na kila mwanadamu huru na mpenda amani analaani na kukemea kwa nguvu zake zote ukatili na vitendo vya kinyama na kigaidi kama hivyo. Hata hivyo inatupasa kukumbusha hapa kwamba, sheria za kimataifa, Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu na hati ya masuala ya kijamii ya Ulaya hazitofautishi baina ya wanadamu na zinauona uhai wa raia wa Nigeria, Syria, Yemeni, Iraqi au Afghanistan kuwa ni sawa na wa raia wa nchi yoyote ya Ulaya au Marekani. Hivyo basi iwapo nchi za Magharibi zisingetofautisha kati ya uhai wa wanadamu na kuchukua msimamo mkali dhidi ya mauaji ya kwa mfano ya wanawake na watoto wa Yemen na kutazama upya mahusiano yao na utawala unaoua watoto wa Saudi Arabia, bila shaka hii leo kusingeshuhudiwa mashambulizi kama haya ya kigaidi katika nchi za Ulaya.