Waislamu Pakistan: Islamabad ijikomboe na utumwa na kuwa tegemezi kwa Marekani
Katibu Mkuu wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu katika jimbo la Sindh nchini Pakistan, ameionya serikali ya nchi hiyo kuwa macho na njama chafu za Marekani.
Allama Maqsood Ali Domki, amesema kuwa umefika wakati kwa Pakistan kujikomboa na utumwa na kuwa tegemezi kwa Marekani kwa sababu Washington haijawahi kuwa rafiki wa kweli wa Pakistan. Sambamba na kusisitiza kuwa, urafiki wa Washington kwa Islamabad ni hatari zaidi ya uadui wake dhidi ya nchi hiyo, Allama Maqsood Domki amesema kuwa, ubalozi wa Marekani nchini Pakistan unajihusisha na ujasusi.
Ameitaka serikali ya nchi hiyo kuufunga ubalozi wa Marekani zikiwemo pia balozi ndogo za nchi hiyo zilizopo Pakistan na kumfukuza pia balozi wa nchi hiyo. Kadhalika Katibu Mkuu wa Majlisi ya Umoja wa Waislamu katika jimbo la Sindh amesema kuwa, siku ambayo balozi wa Marekani atatimuliwa kutoka Pakistan, basi raia wa taifa hilo watafanya sherehe kubwa, kwani Wapakistan sio vibaraka wa Washington wa kuweza kuhatarisha usalama wao kwa maslahi ya Marekani. Hayo yanajiri katika ambayo ni siku kadhaa sasa ambapo raia wa Pakistan wamekuwa wakifanya maandamano mfululizo kupinga siasa na uwepo wa Marekani ndani ya ardhi ya nchi yao.
Stratijia za rais mpya wa Marekani Donald Trump kuihusu Afghanistan na Pakistan ndizo zimepelekea kuibuka hasira kali za raia wa mataifa hayo dhidi ya Washington kiasi cha kutaka askari wa Marekani waondoke katika zao. Katika fremu hiyo, Trump ametishia kuikatia misaada serikali ya Islamabad kwa madai kuwa nchi hiyo inatoa hifadhi kwa makundi ya kigaidi. Weledi wa mambo wanaamini kuwa, madai hayo ya Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Asia yana lengo la kuongeza askari wake ndani ya ardhi ya Pakistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi ambao ni zao la Washington na washirika wake ikiwemo Saudi Arabia.