UNHCR yaomba bajeti kwa ajili ya kuwasaidia Waislamu wa Myanmar
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeomba bajeti kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi wa Kiislamu wa jamii ya Rohingyya wa nchini Myanmar.
Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amesema kuwa, shirika hilo limeomba bajeti ya zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi Waislamu Warohingya.
Afisa huyo wa ngazi za juu wa UNHCR amesema kuwa, shirika hilo linahitajia kiasi cha dola milioni 430 katika kipindi cha miezi sita ijayo kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi Waislamu Warohingyya waliokimbilia katikia nchi jirani ya Bangladesh.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, ukandamizaji na mauaji yanayofanywa na jeshi la Myanmar na mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo ni uangamizaji wa kizazi.
Wakati huo huo, makumi ya mashuirika yya kimataifa yasiyo ya serikali yamesema kuwa hatua za serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya ni jinai za wazi dhidi ya binaadamu ambapo sambamba na kulaani jinai hizo yameitaka dunia kukabiliana na serikali ya nchi hiyo ili kuzuia hali hiyo.
Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wameuawa na maelfu ya wengine wamejeruhiwa tangu kuanza wimbi jipya la mashambulizi ya jeshi na Mabudha wenye misimamo mikali katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi nchi hiyo tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu hadi sasa.