Bush akosoa siasa za kibaguzi za Donald Trump huko Marekani
(last modified Sat, 21 Oct 2017 02:27:19 GMT )
Oct 21, 2017 02:27 UTC
  • Bush akosoa siasa za kibaguzi za Donald Trump huko Marekani

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amesema siasa za nchi hiyo hazipasi kujengeka kwenye msingi wa kujitenga, ubaguzi na urongo.

George Bush ambaye hakutaja waziwazi jina la Donald Trump amesisitiza kuwa, siasa za ugaidi wa kifikra na kinafsi na kuchukua maamuzi kwa mujibu wa dhana tu vinasababisha ukatili na kueneza fikra mgando. 

Bush ambaye alikuwa akimkosoa Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump amesema kuwa, inaonekana kwamba chuki kipofu zinaenea zaidi nchini humo na kwamba sera za Marekani zinasababisha madhara. 

Rais huyo wa zamani wa Marekani amesisitiza kuwa, utambulisho wa Marekani hauarifishwi kwa mujimu wa jiografia, mahusiano ya kidini, damu au ardhi na kwamba chuki na fikra za kibaguzi za wazungu ni doa la aibu kwa Marekani. 

George W. Bush

Akipinga siasa za Trump za kuwapiga vita wahajiri, George W. Bush amezungumzia pia mchango mkubwa wa wahamiaji na umuhimu wa biashara ya kimataifa kwa Marekani. 

Fikra a kibaguzi za Rais Donald Trump wa Marekani zimekabiliwa na upinzani mkubwa ndani na nje ya nchi hiyo.