Kutekelezwa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36017-kutekelezwa_vikwazo_vipya_vya_marekani_dhidi_ya_russia
Serikali ya Marekani imechapisha orodha ya makampuni ya Russia iliyoyawekea vikwazo baada ya kuchapisha sheria mpya ya vikwazo dhidi ya Russia. Katika uwanja huo Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imechapisha orodha inayobainsha sheria hiyo ya vikwazo kuhusu Iran, Korea ya kaskazini na Russia na kutangaza kuyawekea vikwazo makampuni 39 ya kiulinzi na kiitelijinsia ya Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 28, 2017 23:38 UTC
  • Kutekelezwa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya Russia

Serikali ya Marekani imechapisha orodha ya makampuni ya Russia iliyoyawekea vikwazo baada ya kuchapisha sheria mpya ya vikwazo dhidi ya Russia. Katika uwanja huo Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imechapisha orodha inayobainsha sheria hiyo ya vikwazo kuhusu Iran, Korea ya kaskazini na Russia na kutangaza kuyawekea vikwazo makampuni 39 ya kiulinzi na kiitelijinsia ya Russia.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Marekani imeyawekea vikwazo vya darala la pili makampuni 39 ya Russia yanayojihusisha na masuala ya kiulinzi na kiitelijinsia na kwamba makampuni ya Marekani nayo yatawekewa vikwazo iwapo yatashirikiana na makampuni hayo. 

Vikwazo hivyo vipya dhidi ya Moscow vimewekwa licha ya Rais Donald Trump wa Marekani kutoafikiana navyo. Wawakilishi wa vyama viwili vya Democrat na Republican katika Congresi ya Marekani hivi karibuni waliikosoa vikali Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo kwa kupuuza muhula ulioainishwa katika matini ya sheria, kuwepo mapungufu katika kushughulikia agizo hilo na kuituhumu wizara hiyo kuwa ilikaidi kutekeleza vikwazo hivyo dhidi ya Russia. Tarehe Pili Agosti mwaka huu Trump alisaini kuwa sheria mswada wa Congresi unaojulikana kama "Mswada wa Kukabiliana na Maadui wa Marekani kupitia Vikwazo" - Countering America’s Adversaries Through Sanctions Act (CATSA) ambao ulitaka kuwekewa vikwazo vipya Iran, Russia na Korea Kaskazini. Trump aliutaja mswada huo kuwa kosa kwa sababu unampunguzia mamlaka ya kupunguza vikwazo dhidi ya Russia na kwa msingi huo hakutaka kuusaini, hata hivyo uungaji mkono mkubwa wa wabunge wa vyama vyote viwili katika Congresi ya Marekani ulimfanya asiwe na chaguo jingine isipokuwa kuutia saini. Kwa utaratibu huo, inaonekana kuwa uhusiano wa Russia na Marekani umeingia katika marhala mpya ya mivutano huku Dimitry Paskov Msemaji wa Ikulu ya Russia (Kremlin) akitaja faharasa hiyo ya vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya nchi yake kuwa ni ishara ya kuendelea siasa za kiuhasama za Washington dhidi ya Moscow. 

Rais Donald Trump wa Marekani akisaini mswada kuwa sheria dhidi ya Russia Agosti 2, 2017

Alex Mukhin mchambuzi wa kisiasa wa Russia anaamini kuwa waandaaji wa vikwazo vipya dhidi ya Russia nchini Marekani wamefanya kosa kubwa. Mwenendo wa hali ya mambo sasa unaonekana kuwa tofauti kikamilifu na ilivyotarajiwa, na kinyume na mtazamo wa awali wa viongozi wa Russia kwamba uhusiano kati ya Moscow na Washington ungeimarika baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump. Katika hali ambayo Trump amekuwa akitaka kuimarisha uhusiano na Russia na hata kushirikiana nayo katika baadhi ya masuala ya kimataifa, lakini njia ya kuboresha uhusiano wa pande mbili hizo imefungwa kufuatia hatua ya Congresi ya Marekani ya kuongeza vikwazo dhidi ya Russia, hatua ambayo hata hivyo imeungwa mkono na White House.

Hivi sasa tunashuhudia ukinzani wa wazi kati ya mfumo wa uongozi wa Marekani na serikali ya Trump ambao marejeo yake ni congresi kuhusu namna ya kukabiliana na Russia. Sheria ya vikwazo dhidi ya Russsia imefunga kila njia ya kuboresha uhusiano wa Marekani na Russia, bali itazidisha tu mivutano kati ya pande mbili hizo. Kwa kuzingatia vikwazo hivyo vipya na pia kuendelea hitilafu na migawanyiko katika misimamo ya Moscow na Washington kuhusiana na masuala mengi ya kimataifa khususan mgogoro wa Syria na Ukraine na vile vile congresi ya nchi hiyo kuendeleza chuki zake bila kificho ikitaka kushadidisha misimamo ya Washington dhidi ya Moscow, yote hayo yameondoa matumaini ya kurekebishwa hali iliyopo na kuanza awamu mpya katika uhusiano wa Marekani na Russia. Kuendelea hatua za kiuhasama za Washington dhidi ya Moscow kunaonyesha kuwa viongozi wa Marekani wamedhamiria kuisababishia Russia changamoto mbalimbali; suala ambalo linafuatiwa na radiamali na hatua mkabala kutoka Moscow. Sergey Rogov Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Kirussia anaamini kuwa: Vita baridi vinajiri hii leo baina ya Russia na Marekani. Uzoefu wa huko nyuma unaonyesha kuwa Warussia si tu kuwa wamekuwa wakakamavu mbele ya mashinikizo mengi kama hayo ya Marekani bali wamechukua pia hatua mkabala na vitendo hivyo vya kiuadui vya Washington.  

Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Siasa katika Akademia ya Marekani na Canada