Katibu Mkuu wa Ansarullah Yemen: Marekani inashiriki kuikalia kwa mabavu Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37321-katibu_mkuu_wa_ansarullah_yemen_marekani_inashiriki_kuikalia_kwa_mabavu_palestina
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa Washington inashirikiana na utawala wa Kizayuni kuikalia kwa mabavu Palestina.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Dec 08, 2017 01:17 UTC
  • Katibu Mkuu wa Ansarullah Yemen: Marekani inashiriki kuikalia kwa mabavu Palestina

Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa Washington inashirikiana na utawala wa Kizayuni kuikalia kwa mabavu Palestina.

Sayyid Abdulmalik al Houthi amewatolea wito wananchi wa Yemen leo Ijumaa kumiminika mitaani kulaani hatua ya Marekani ya kuitangaza Quds kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni. 

Miji mbalimbali ya nchi za Kiislamu imeshuhudia maandamano ya wananci baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutangaza uamuzi wake huo huku leo hii Iran ikifanya maandamano kulaani hatua hiyo ya Rais wa Marekani. Jumatatu ijayo maeneo mbalimbali ya Lebanon yatashuhudia maandamano ya wananchi dhidi ya Marekani. 

Jana Alhamisi wakazi wa Ukingo wa magharibi wa Mto Jordan, Ukanda wa Ghaza, Jordan na kusini mwa Lebanon pia walifanya maandamano kulalamikia hatua ya Rais Trump ya kuutangaza mji wa Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni.

Wakazi wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza katika maandamano dhidi ya Trump

Hatua hiyo ya Rais wa Marekani imekabiliwa na upinzani mkubwa wa nchi za Kiislamu na kukosolewa pakubwa kimataifa.