Putini afichua ushirikiano wa Marekani na magaidi huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i37655-putini_afichua_ushirikiano_wa_marekani_na_magaidi_huko_syria
Rais wa Russia amefichua kuwa wanajeshi wa Marekani walioko nchini Syria walikuwa wakiwaunga mkono na kuwapatia silaha magaidi na ndio waliokuwa wakikwamisha kusambaratishwa magaidi hao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 16, 2017 03:45 UTC
  • Putini afichua ushirikiano wa Marekani na magaidi huko Syria

Rais wa Russia amefichua kuwa wanajeshi wa Marekani walioko nchini Syria walikuwa wakiwaunga mkono na kuwapatia silaha magaidi na ndio waliokuwa wakikwamisha kusambaratishwa magaidi hao.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Vladimir Putin ameashiria hatua ya Marekani ya kuyatumia makundi ya kigaidi na kueleza kuwa: Wanajeshi wa Marekani nchini Syria walijizuia kuendesha mapambano na kuwaangamiza magaidi nchini humo na ndio maana magaidi walinusurika kuuawa kutokana na hatua hizo za wanajeshi wa Marekani. 

Rais Vladimir Putin wa Russia 

Rais wa Russia ameongeza kusema kuwa, picha za droni za kijasusi za nchi hiyo zinaonyesha kuwa, magaidi wanakimbilia Iraq wakitokea katika mipaka ya Syria. Rais Putin amesema, wanajeshi wa Russia waliripoti suala hilo kwa wenzao wa Marekani sambamba na kuwajulisha njia zinazotumiwa na magaidi hao; hata hivyo wanajeshi wa Marekani hawakuchukua hatua yoyote.

Putin anesena wanajeshi wa Marekani wanadhani kwamba wanaweza kuwatumia magaidi hao nchini Syria kupambana na utawala wa Rais Bashar al Assad.

Russia kwa mara imekuwa ikiikosoa Marekani kwa kuyaunga mkono kwa hali na mali makundi ya kigaidi huko Syria lengo likiwa ni kufanikisha maslahi yake katika nchi hiyo ya Kiarabu. Aidha Marekani na nchi waitifaki wake wa Kiarabu na Magharibi ni miongoni mwa nchi zinazolifadhili kifedha na kisilaha kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.