Baraza la Haki za Binadamu la UN lakosoa jinai za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/world-i39425-baraza_la_haki_za_binadamu_la_un_lakosoa_jinai_za_israel
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeukosoa vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai unazowafanyia wananchi madhulumu wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 24, 2018 10:33 UTC
  • Baraza la Haki za Binadamu la UN lakosoa jinai za Israel

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeukosoa vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai unazowafanyia wananchi madhulumu wa Palestina.

Katika mkutano uliofanyika mjini Geneva, baadhi ya nchi wanachama wa baraza hilo zimeitaja Israel kuwa ni utawala wa kibaguzi (apartheid). Mjumbe wa Afrika Kusini katika baraza hilo ameongoza wimbi la kukashifu jinai wanazofanyiwa Wapalestina na utawala haramu wa Israel, na kusema kuwa Israel ndio utawala wa kipekee wa kibaguzi duniani.

Mwakilishi wa Palestina katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Dima Asfour ameitaka Israel kutamatisha miaka 50 ya kukalia kwa mabavu ardhi ya Palestina.

Jinai za wanajeshi wa Israel dhidi ya Wapalestina

Amesisitiza kuwa, wananchi wa Palestina hawataachana na jitihada na mapambano ya kupigania haki zao na ardhi yao.

Iran, Jordan, Imarati, Russia, Malaysia na nchi nyingine wanachama wa baraza hilo zimeutaka utawala batili wa Israel uheshimu sheria za kimataifa kwa kuacha ukaliaji wa mabavu, ukoloni na mfumo wa kibaguzi dhidi ya Wapalestina.

Uingereza, Finland na Austria miongoni mwa nchi nyingine zilizoshiriki mkutano huo wa Geneva zimevitaka vyombo vya usalama vya Israel vikomeshe tabia ya kuwatia mbaroni watoto wadogo wa Kipalestina.