Mar 12, 2018 07:24 UTC
  • Amnesty International : Jeshi la Myanmar linatwaa maeneo ya Waislamu Warohingya

Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International unaonyesha kuwa, jeshi la Myanmar limejenga kituo katika vijiji ambavyo Waislamu wa jamii ya Rohingya wamelazimishwa kuyakimbia makaazi yao.

Wanaharakati wa shirika hilo wamesema kuwa, watu walioshuhudia na uchunguzi uliofanywa kupitia picha za satalaiti unaonyesha kwamba, mwezi Januari wanajeshi wa Myanmar walikuwa wakisawazisha ardhi ya vijiji vya  Waislamu wa jamii ya Rohingya  kwa kubomoa nyumba na hivi karibuni wamechoma moto eneo hilo.

Tirana Hassan, msemaji wa Amnesty International ameelezea hatua zillizochukuliwa katika jimbo la Rakhine kwamba ni ''Jeshi kujinyakulia ardhi''.

Serikali ya Myanmar bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na ripoti hiyo ya Shirika la Msamaha Duniani la  Amnesty International.

Waislamuu Warohingya wakiyahama makazi yao

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alielezea wasi wasi mkubwa alionao kwamba yumkini mauaji ya kimbari yamefanywa dhidi ya Waislamu wa Rohingya nchini Myanmar tangu Agosti mwaka jana 2017.  

Maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa, mbali na wengine zaidi ya laki saba kulazimishwa kukimbilia katika nchi jirani ya Bangladesh, tangu Agosti 25 mwaka jana, lilipoanza wimbi jipya la mashambulizi ya jeshi na Mabudha wenye misimamo mikali katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa nchi nchi hiyo. 

Walimwenguu wameendelea kuukosoa Umoja wa Mataifa kutokana na kutochukuua hatua zozote za maana kukomesha jinai na mauaji dhidi ya Waislamu hao wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar.

Tags